katika hali isiyokuwa ya kawaida siku ya leo wakazi wa mbagala wamejikuta wakiingia katika sekeseke la aina yake baada ya kulipuka kwa Vurugu kubwa iliyokuwa ikifanywa na wananchi wenye Imani ya Kiislam kwa madai kuwa mtoto toka familia ya Kikristo alikuwa amefanya kitendo cha kukashifu dini ya kiislam baada kukojolea kitabu cha dini hiyo "Quran"
wakazi wa mbagala wakiwa katika hali ya sekeseka huku askari wa kutuliz ghasia FFU wakiwa wameshawasili eneo la tukio kuweka hali ya usalama na kuzuia uharibifu uliokuwa ukifanywa na wananchi hao |
Licha ya kitendo hicho kudaiwa kufanywa na mtoto mdogo wa eneno hilo wananchi hao wenye imani ya Kiislam walielekeza hasira zao kwa kuanza kuchoma makanisa ikiwa ni pamoja na kanisa la TAG na kanisa la KKKT ,kanisa la sabato na kanisa catholic yote ya eneo hilo la mbagala
kwa mujibu wa chanzo kimojawapo cha habari inasemekana kwamba mbali na kuchoma moto makanisa hayo matatu watu hao pia wamevunja magari
yaliyokuwa maeneo ya makanisa hayo na pia walikuwa wanamtaka mtoto anaedaiwa kufanya kitendo hicho cha kukojelea Quran wapewe wao.
wakati vurugu hizo zikiendelea ghafla askari wa
kutuliza ghasia FFU walifika eneo hilo la tukio na kuanza kufyatua
mabomu ya kutoa machozi kwa lengo la kutawanya watu hao walikuwa
wakiendelea na uharibifu huo wa makanisa
tutaendelea kukufahamisha kadri tunavyozidi kupata taarifa zaidi toka hapo mbagala.,......
hali ya tukio zima ni kama inavyoonekana katika picha zilizopigwa na Gerlad Kimanga MS coner
baadhi ya wakazi wa eneo hilo la Mbagala wakiwa katika sintofaham kutokana na vurugu hizo zilizoibuka ghafla eneo hilo la mbagala |
Polisi wa kutuliza ghasia wakionekana kwa mbali katika moja ya operation walizokuwa wakifanya kurudisha hali ya usalama eneno hilo |
Kutokana na vurugu hizo za waislam wenye itikadi kali kitendo hicho pia kimeathiri mwenendo mzima wa masomo katika eneno hilo huku baadhi ya watoto wadogo wanafunzi wa shule wakionekana kuathiriwa vibaya na mabomu ya machozi yaliyokuwa yanalipuliwa kuwatawanya watu hao waliokuwa wameelekea pia katika kituo cha polisi wakimtaka mtuhumiwa wao
hawa ni baadhi ya watoto waliopatwa na madhara ya mabomu ya machozi eneno hilo la mbagala |