Jumapili hii mchekeshaji maarufu toka kundi la ze Comedy Masanja Mkandamizaji alikua ni moja ya wahamasishaji katika kuchangia fedha zinazotarajiwa kutumika katika upanuzi wa Kanisa la EAGT Lumala mpya kwa pastor Dr. Daniel Kulola.
katika upanuzi wa kanisa hilo inakadiriwa kuwa kanisa hilo baada ya upanuzi litaweza kuchukua idadi ya watu 2000 hadi 5000 kwa ibada moja
gharama za ujenzi wa kanisa hilo hadi kukamilika zinatarajiwa kufikia Shilingi Milion 250 hadi Milion 300 fedha za kitanzania.
kwa mujibu wa Mchungaji wa kanisa hillo Pastor.Dr.Daniel Kulola hili ndilo tamko lake kuhusu ujenzi huo wa kanisa jipya
""""Ndg marafiki na wapendwa wote
mimi mch Dr. Daniel Moses Kulola na kanisa lote la E.A.G.T Lumala mpya Mwanza
tumechoresha ramani hii ili kulipanua kanisa letu kwani kwa sasa halitoshi
kabisa... Tunakuomba ushirikiane nasi katika maono haya mazuri na ya kimungu
kabisa katika kuchangia baraka hizi... Wote waliofanya kazi na Mungu hawakubaki
kama walivyo Mungu aliwainua kabisaa...
Tunaomba kama utaguswa
kutusaidia ingalau vifaa vya ujenzi, fedha, dhahabu waweza kuwasiliana na mch
kwa namba zake za simu lakini pia kama utaweza tuma kwenye akaunti ya kanisa: Evangelistic Assemblies of God (T)
Mwanza , bank ya KCB tawi la mwanza Tanzania
account number ni 0200509975 na swift code: KCBL TZ
|
Pastor Dr.Daniel kulola |
ukituma wasiliana na mch ili kutunza kumbukumbu na kutuma barua ya asante
kwako. Ukitaka kufika ili uone ujenzi basi fuata maelekezo
mtu akifika mwanza anaweza akafika nyuma ya soko jipya la saba saba barabara la
kwenda Airport Mwanza. Na ukitaka kutuma kwa M-pesa tumia namba za mch Dr.
Daniel Moses Kulola za simu +255 767 749040 na Airtel money ni +255784 784
749040 E-mail ya mch ni pastordanielkulola@yahoo.com
au
Pastor Dr. Daniel Moses Kulola
Evangelistic Assemblies of God Tanzania
E.A.G.T Lumala mpya church
P.O. Box 30, Postal rd,mwanza, Tanzania (E.A)
sehem ya ramani ya kanisa hilo ambalo linatarajiwa kujengwa ni kama inavyoonekana katika picha hapa chini
katika kuhamisha uchangiaji wa ujenzi huo msanii Masanja mkandamizaji alikuwepo katika kuendesha harambee na zoez lilikuwa kama linavyoonekana kwenye picha hapa chini
|
Masanja Mkandamizaji akiwahamasisha waumini katika kuchangia harambee hiyo ya upanuzi wa kanisa |
Kutazama video ya Masanja alivyokuwa akiperfom siku hiyo bofya hapo chini
|
palikua hapatoshi wakati huo kila mtu akasimama ili aone kinachoendelea |
|
Sehem ya waumini wakitazama masanja akiimba nyimbo zake ndani ya kanisa siku hiyo |
|
wakati huohuo Masanja na vijana wake wa kazi tok Mito ya baraka Dar es salaam wakapata fursa ya kufanya vitu vyao |
|
hii ni sehem ya kanisa kwa sasa linavyoonekana |
|
Bwana Yesu Asifiweeeeeeee |
|
Pastor.Dr.Daniel Kulola akifafanua jambo na Masanja mkandamizaji |
|
Khaaa mama hicho kiasi kidogo hivyooooo hebu ongeza banaaa |
|
Je ungepeeeeenda nisemeeeeeeee |
|
Masanja Mkandamizaji akisisitiza jambo katika harambee hiyo |
|
sehem ya waumini waliohudhuria siku hiyo |
|
watoto wadogo nao pia walikuwa wakichangia japo kwa kiasi kidogo walichokuwa nacho |
|
mmoja wa washirika akitoa ahadi yake katika kuchangia ujenziwa kanisa hilo |