Mchungaji na mwanasiasa wa siku nyingi maarufu kama Christopher Mtikila ambaye amekuwa mstari wa mbele katika harakati za kisiasa na uchungaji sambamba na mambo ya kisheria ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.
Mchungaji Christopher Mtikila ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha Democratic Party (DP)alikua akikabiliwa na mashtaka mahakamani kwa kudaiwa kutoa maneno yenye uchochezi,dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais, maneno ambayo alidaiwa kuyatoa mwezi oktoba 21 mwaka jana katika maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam
baada ya kupata ushindi dhidi ya kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mchungaji Christopher Mtikila hiki ndicho alichokisema
“Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu”.
Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.
Mchungaji christopher Mtikila haishiwi na vioja kila kukicha alivuma sana tangu enzi za mwalimu na na sera za ugabachori na hadi sasa mchungaji huyo amekuwa haishi kutinga mahakamani kwa kesi mbali mbali kwa kile anachokiita mwenyewe kupigania haki na uhuru wa wa Taifa la Tanganyika ambalo unadhulumiwa na baadahi ya wanasiasa nchini Tanganyika
Tazama Habari hii zaidi kama ilivyorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV hapa chini
Mchungaji Christopher Mtikila ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha Democratic Party (DP)alikua akikabiliwa na mashtaka mahakamani kwa kudaiwa kutoa maneno yenye uchochezi,dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais, maneno ambayo alidaiwa kuyatoa mwezi oktoba 21 mwaka jana katika maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam
baada ya kupata ushindi dhidi ya kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mchungaji Christopher Mtikila hiki ndicho alichokisema
Mara baada ya ushindi wa kesi hiyo kesi hiyo lilizuka sakata lingine liliibuka baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report Book) akimtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa viwanja.
Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.
Mchungaji Christopher Mtikila akiwa katika moja ya mikutano yake ya siasa |