hatimaye Iran imemuachia mchungaji Youcef Nadarkhan baada ya kumshikilia kwa muda wa miaka mitatu jela kutokana na kumtuhumu kwa makosa ya utume nchini humo.
awali mwanzoni mwa mwezi february mwaka huu nchi ya Irani ilitoa adhabu ya kifo kwa mchungaji huyo kunyongwa hadi kufa kutokana na kukutwa akifanya shughuli za uinjilishaji na kuhubiri injili ya Yesu kristo katika nchi hiyo ambayo ni nchi ya kiislam na inayoongozwa kwa sheria za kiislam.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa jarida la Fox News, Jordan Sekulow, na kiongozi wa mtandao wa ACJL amethibitisha taarifa za kuachiliwa kwa mchungaji Youcef Nadarkhan kuwa ni kweli na kuweka picha katika mtandao wa Tweeter zinazomwonyesha mchungaji huyo akiungana tena na familia yake siku ya jumamosi ya tarehe 8september 2012 baada ya kutengana nayo kwa muda wa miaka mitatu kipindi alipokuwa gerezani .
Nadarkhani, raia wa Iran na mchungaji kutoka katika huduma ijulikanayo kama network of house churches, alikamatwa Oct. 13, 2009, baada ya kupinga uamuzi wa serikali ya Iran kuwalazimisha watoto wote nchini Iran akiwemo na mtoto wake kusoma Quran. na pia kwa kosa la kutaka kufungua kanisa katika nchi hiyo ya kiislam.
kutokana na makosa hayo Nadarkhan alihukumiwa adhabu ya kifo mwaka 2010
Katika mahakama ya nchi hiyo siku ya tarehe 8september mwaka huu kesi ya Nadarkhan ilidumu kwa muda wa masaa sita lakini mwisho mahakama hiyo ilimuachilia huru Mchungaji huyo.
Moja ya mtandao wa ujulikanao kama ACJL na ambao ulizindua kampeni kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kuishinikiza serikali ya Iran kumwachilia mchungaji huyo, umesema kwamba Nadarkan alikutwa na makosa ya kufanya Uinjilist kwa Waislam kosa ambalo kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo ni kifungo cha miaka mitatu jela hivyo kwa kipindi chote cha miaka mitatu ambacho mchungaji huyo amekuwa gerezani mda wa kifungo hicho umeshamalizika
katika moja ya kauli za mchungaji Nadarkhan alikaririwa akisema wapendwa wangu "japo kesi yangu imechukua mda mrefu ,kimwili natamani siku ziishe, lakini nimejikabidhi kwa Mungu na mapenzi ya Mungu yatimie"
Mara baada ya kuachiliwa huru mchungaji Youcef Nadarkhan kauli yake kwa wakristo wote duniani amenukuliwa akisema "Nawashukuru wote kwa sapoti mliyonipa kupitia maombi yenu"
Jason DeMars,mwanzilishi na Kiongozi wa huduma ya "Present Truth Ministries" ambayo mchungaji Nadarkhan amekuwa akifanya nayo kazi katika huduma yake ya kitume amenukuliwa akisema kuwa "Tunamshukuru Mungu kwa Deliverance ya mchungaji Nadarkhan na pia kwa kujibu maombi yetu"

Mchungaji Youcef Nadarkhan akiungana na familia yake mara baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya nchi ya Iran |