Kiongozi na Mchungaji wa Kanisa la Mwanza International Community Church lililopo jijini Mwanza, Zakayo Nzogere na Carol Nzogere wa MICC ameendelea kuwaunganisha waumini kwa pamoja katika kutimiza wito wa kujenga jengo la aina yake na la kisasa la kanisa ambapo waumini wengi jijini Mwanza watapata nafasi ya kumwabudu Mungu kwa nafasi ya kutosha na kwa Ubora wa viwango vya juu.
Katika moja ya kauli zake ambazo Blog hii iliwahi kumnukuu
kiongozi wa kanisa Hilo,Zakayo Nzogere aliwahi kusema
"Mungu wetu sio mganga wa kienyeji kanakwamba tufanye ibada zetu kienyeji enyeji kwenye majengo ya kienyeji enyeji na kwa utaratibu wa kienyeji enyeji,Mungu wetu ni mkubwa na mwenye Heshima na Utukufu wa hali ya juu kupita vyote hivyo hata tunasema tunataka kumwabudu inatupasa kumwabudu Mungu katika Jengo la kisasa lenye Ubora na lenye Hadhi hata ya kusema hapa ndipo watoto wake wanapomwabudia Mungu wao.
kwa kulitimiza hilo kwa Vitendo ujenzi wa kanisa umetimiza miezi mpaka sasa tangu ulipoanza mnamo tarehe 22June2015, na mpaka sasa mwezi September 22.
katika moja ya post toka kwenye ukuras wa facebook wa kanisa hilo blog hii imenukuu yafuatayo kama yalivyoandikwa
MIEZI MITATU YA UAMINIFU WA MUNGU (June 22 - September 22): Kwa msaada wa MUNGU tulianza mradi huu mkubwa wa kujenga kanisa la MICC Jijini Mwanza. Tumefikia hatua ya kupaua. Katika hatua hii tunapenda kuomba mchango wako ili tukamilishe kupaua jengo. Je, Waweza kuchangia kazi hii angalau elfu kumi (10,000)? Waweza changia kupitia MPESA, TIGO PESA & AIRTEL MONEY. Ubarikiwe!
baadhi ya picha za ujenzi wa kanisa hilo ni kama zinavyoonekana hapa