Askofu John Peter Bigirimana Amewataka wakristo kujikita zaidi katika maombi ili waweze kuzipambanua roho na huduma mbali mbali kama zatoka kwa Mungu au la...
Askofu Bigirimana amesisitiza kuwa kwa mtu mwenye Hofu ya Mungu na anayeishi katika uwepo wa Mungu si rahisi kudanganywa na manabii wa uwongo ambao wameibuka kwa kasi katika kipindi hiki duniani kote..
"Solution ya matatizo yote haya ya kuwepo na wimbi kubwa la manabii wa uwongo ni watu kuwa waombaji" alisema Bishop Bigirimana
hivi sasa kutokana na upendo kwa wengi kupoa,na baadhi ya watumishi kutojishughulisha katika Kumtafuta Mungu kwa njia zilizopo kwenye Biblia, baadhi wamekuwa wakidaiwa kutumia nguvu za giza lengo likiwa ni kupata umaarufu kwa njia za kuwa na miujiza ya uponyaji katika huduma zao, ambao Bigirimana ameufananisha na mazingaombwe akienda mbali zaidi kwa kusema si kweli kwamba uponyaji ule unaopatikana toka kwa manabii hao wa uwongo hua ni uponyaji wa kudumu.
katika mahojiano maalum na blog hii siku ya mwisho baada ya conference ambapo Askofu Bigirimana alikuwa akifundisha mafundisho mbali mbali ya kiroho jijini Mwanza ,
conference iliyofanyika katika kanisa la EAGT Lumala mpya, Askofu Bigirimana emeeleza kuwa
hali ilivyo sasa ni tofauti sana na miaka ya 1980 ambapo hali ya kiroho kwa wakristo wengi ilikua ipo juu sana tofauti na sasa ambapo giza la kiroho limetanda katika nchi nyingi.
baadhi ya wakristo waliowengi wamejikuta wanashikilia mambo ya asili ikiwa ni pamoja na chuki baina yao,magawanyiko,ugomvi baina yao,tamaa ya mapato,huduma imekuwa vyeo na mambo mengi ambayo hayampendezi Mungu...
"kwa mfano hali ilivyo sasa kwa upande wa waimbaji wa nyimbo za injili ,muimbaji hadi aje kuimba kwenye huduma yoyote lazima apate malipo kwanza ndipo aje aimbe vinginevyo haji kuimba".
Askofu Bigirimana aliingia Tanzania miaka ya 1973 akitoke nchini Burundi hadi 1988 na kuhamia nchini Norway ambapo huduma yake ijulikanayo kama Reach Nations Outrich ministries.
hadi sasa huduma yake imekuwa na kwa kiasi kikubwa kwa kuweza kufungua matawi katika nchi mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na ,Malawi,Kongo,Burundi,Ivory coast ,America,Australia,Belgium,Zambia,Mozambique,
katika kuhitimisha mazungumzo na blog hii Askofu Birigimana alibainisha kuwa kwa sasa amemua kujikita zaidi barani afrika ambapo wito wake sasa umejikita zaidi katika kuwahubiria waafrika wenzake wamjue Mungu wa kweli kwani hivi sasa Mwili wa Kristo umechanika chanika sana kutokana na kuwepo kwa migawanyiko mingi sana katika makanisa.
wakristo watafute kanisa litakalowafikisha mbinguni ,kanisa linalomhubiri Yesu Kristo katika kweli kama Biblia inavyosema
hapa chini ni picha za mapokezi ya Bishop Bigirimana alipowasili jijini Mwanza na namna OYES conference ilivyofanyika katika kanisa la E.A.G.T Lumala mpya
Askofu John Peter Bigirimana |

Mahojiano yangu na Bishop Bigirimana toka Norway yaliyofanyika nyumbani kwa Mwinjilist Dr.Daniel Moses Kulola |

Mrs.Kihoza mmoja wa waalimu wa ujasiriamali ambapo ilikua ni moja ya mafundisho yaliyokuwa yanatolewa katika conference hiyo |
Bishop Bigirimana akiwasili Airport ya Jiji la Mwanza na kupokelewa na mwenyeji wake Pastor,Dr.Daniel Moses Kulola |
Deliverance |