Jumapili hii ya tarehe 2September Blog hii ilitupia jicho lake katika moja ya huduma inayokuwa kwa kasi kubwa hapa jijini Mwanza ambayo ni katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya Mwinjilist wa Kimataifa na Mtoto wa Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT nchini Tanzania huyu si mwingine bali ni Dr.Daniel Moses Kulola
wengi walizoea kumuona katika majukwaa makubwa akihubiri kama muinjilist lakini kwa sasa Mtumishi huyu wa Mungu kwa sasa anafanya pia huduma ya Kichungaji ambapo kwa sasa anahudumu pia kama mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT Lumala mpya lililopo Ilemela,jijini Mwanza karibu na soko maarufu la SABASABA
huduma hii imekuwa kwa kasi ya ajabu katika kipindi kifupi na na watu wamekuwa wakimiminika kwa wingi kila jumapili kwenda kumuabudu Mungu mahali hapo.
sehem ya shughuli za ibada zinavyofanyika kanisani hapo ni kama inavyoonekana katika picha hapa chini ambapo hii ilikua ni jumapili ya tarehe 2September 2012
|
Mch.Dr. Daniel Moses Kulola akiwakaribisha wageni ambao walikuwa wamefika kwa mara ya kwanza kanisani hapo |
|
Hii ni view ya kanisa ikionyesha sehem ya waumini ambao hukusanyika mahali hapo kuabudu | |
|
Mch.Dr.Daniel Moses Kulola akifafanua jambo kanisani hapo |
|
Mbele ni wageni ambao walikuwa wamefika kwa mara ya kwanza katika kanisa hili |
|
Mch.Dr.Daniel Moses Kulola akimsikiliza kwa makini mmoja wa wageni waliofika kwa mara ya kwanza kanisani hapo |
|
Mama mchungaji Daniel Kulola,,,anajulikana kama Mrs.Mercy Kulola |
|
Mr.Zoka na mkewe wakiwa katika kutoa shukurani kanisani hapo kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa |
|
Sehem ya waumini wakitoa shukurani madhabahuni hapo kwa kupata Baraka za watoto baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na watoto |
|
Mchungaji wa kanisa hilo la EAGT Lumala Mpya Dr.Daniel Moses Kulola akiachia tabasamu zito wakat akimsikiliza mmoja wa wageni waliokuwa wakijitambulisha kanisani hapo siku hii ya jumapili |
|
Mrs.Mercy Kulola mama mchungaji wa kanisa hili |
|
Mch.Dr.Daniel Moses Kulola na mkewe Mrs.Mercy Kulola wakifanya maombezi kwa mtoto mchanga ambaye ni muujiza toka kwa Bwana baada ya wazazi wake kukaa kwa kipindi kirefu bila kuwa na mtoto |
|
Mch.Dr.Daniel Moses Kulola akihubiri katika Ibada iliyofanyika siku hiyo |