Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika wizara ya fedha na kukagua utendaji kazi, akuta wafanyakazi wengi hawapo kazini.
Rais Magufuli amefanya ziara hiyo fupi kutoka ikulu muda mfupi baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju.
Bw Masaju aliteuliwa mara ya kwanza kuwa Mwanasheria Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Januari mwaka huu baada ya kujiuzulu kwa George Werema.
Bw Magufuli hakuzungumza rasmi na wanahabari baada ya kumaliza ziara hiyo.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema kuna uwezekano amezungumza na maafisa wa hazina kuu kuhusu hali ya mikopo ya wanafunzi.
Wakati wa kampeni, Bw Magufuli aliahidi kufanya elimu kuwa bila malipo kuanzia shule za msingi hadi shule za sekondari.
Bw Magufuli ameagiza Bunge lifunguliwe Novemba 17 na anatarajia kuwasilisha jina la Waziri Mkuu wake kwa bunge hilo Novemba 19.
Rais Magufuli katikia ziara yake hiyo ya kustukiza kwenda Wizara ya fedha imefanyika kwa kutembea kwa miguu toka Ikulu jijini Dar es Salaam mpaka wizara ya fedha na kufanya ukaguzi wa ghafla chumba hadi chumba,Aidha wengi wa maofisa na wafanyakazi katika wizara hiyo walikua hawapo maofisini.
Rais Magufuli amefanya ziara hiyo fupi kutoka ikulu muda mfupi baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju.
Bw Masaju aliteuliwa mara ya kwanza kuwa Mwanasheria Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Januari mwaka huu baada ya kujiuzulu kwa George Werema.
Bw Magufuli hakuzungumza rasmi na wanahabari baada ya kumaliza ziara hiyo.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema kuna uwezekano amezungumza na maafisa wa hazina kuu kuhusu hali ya mikopo ya wanafunzi.
Wakati wa kampeni, Bw Magufuli aliahidi kufanya elimu kuwa bila malipo kuanzia shule za msingi hadi shule za sekondari.
Bw Magufuli ameagiza Bunge lifunguliwe Novemba 17 na anatarajia kuwasilisha jina la Waziri Mkuu wake kwa bunge hilo Novemba 19.
Sehemu ya picha za ziara hiyo ya ghafla ya Rais Magufuli,kama ilivyonaswa na watu mbalimbali kwa kupiga picha kwa kutumia simu zao za mikononi,,,nimekuwekea hapa chini..