Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiagiza Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kufanya upembuzi yakinifu kisha kuwarejeshea fedha zao wananchi waliokuwa wamewekeza katika Kampuni ya Kusimamia shughuli za Upatu, kwa mtindo wa kupanda na kuvuna fedha (Deci).
Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana alisoma hukumu hiyo kwa niaba ya Hakimu Mkazi, Stuart Sanga ambaye ndiye aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyowahusisha wakurugenzi watano wa Deci.
Wakati Mahakama hiyo ikiamuru wanachama hao wa Deci walipwe, wakurugenzi wanne wa Deci kati ya watano ambao walishtakiwa katika kesi hiyo walipatikana na hatia ya kuendesha shughuli za upatu bila kuwa na leseni. Mmoja aliachiwa huru.
Waliopatikana na hatia ni Jackson Sifael Mtares, Dominic Kigendi, Samuel Sifael Mtares na Timotheo Ole Loitingye ambao wote ni wachungaji wa makanisa tofauti ya Kipentekosti na mshtakiwa aliyeachiwa huru ni Arbogast Kipilimbi ambaye alikuwa mhamasishaji wa Deci.
Hakimu Katemana aliwahukumu washtakiwa hao kulipa faini ya jumla ya Sh84 milioni wote kwa pamoja, ikiwa ni Sh21 milioni, kwa kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Hata hivyo, washtakiwa wawili Jackson Mtares na Ole Loitingye walilipa faini hiyo na kuachiwa huru, huku wenzao Samuel Mtares na Dominick Kagendi wakipelekwa gerezani kuanza kutumikia adhabu ya kifungo baada ya kushindwa kulipa.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Katemana alisema baada ya kusikiliza mashahidi 16 wa upande wa mashtaka (Jamhuri) na vielelezo 27 pamoja na ushahidi wa utetezi wa washtakiwa, Mahakama imeridhika kuwa washtakiwa hao wanne wana hatia kwa makosa yote mawili.
Wakati washtakiwa hao walipokamatwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), aliwasilisha mahakamani hati ya kuomba mali zote zilizoshukiwa kuhusiana au kumilikiwa na Deci, kama vile akaunti za benki, majengo na magari, zikamatwe na kushikiliwa hadi kesi itakapoisha.
Katika hukumu yake jana, Hakimu Sanga alisema baada ya kuchambua ushahidi wa pande zote imebainika kuwa kuna mali ambazo zilikamatwa lakini hazikuwa za Deci.
Aliamuru mali hizo zirejeshwe kwa wenyewe na hasa fedha zilizokuwa zimewekezwa na wanachama. Aliiagiza Serikali kupitia BoT, kufanya uchambuzi yakinifu na kisha kuwarejeshea wanachama waliokuwa wamepanda mbegu ambao walikuwa bado hawajavuna, baada ya kuwasilisha ushahidi wa vielelezo muhimu.
Alisema kuwa ikiwa fedha hizo hazitatosha, mali mbalimbali za Deci zilizokamatwa zitauzwa ili kufidia malipo ya wanachama hao.
Awali, baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Prosper Mwangamila alidai kuwa upande wa mashtaka hauna kumbukumbu za makosa ya jinai kwa washtakiwa.
Source: Mwananchi