Chuo kipya cha Muziki wa Injili chenye makazi yake Sinza Kumekucha jijini Dar es Salaam,ni moja ya kituo ambacho kimekua kama Kiwanda cha kutengeneza Viwango vya wanamuziki wa injili kuanzia Sauti za waimbaji mpaka wapiga vyombo vya Muziki.
Katika Harakati za kuukuza Muziki wa Tanzania na kuupandisha kimataifa Chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo kwa waimbaji na wanamuziki ikiwa ni pamoja na Sauti na namna ya Kuimba,Upigaji wa vyombo ikiwa ni pamoja na Guiter,Piano, Upigaji Drums na mafunzo mengine mengi zaidi ya kiroho kwa wanamuziki wa injili
Miongoni mwa waratibu na walimu wa chuo hiki cha New Gen Music School ni pamoja na Daniel Mfwango,Bomby Johnson,Amani Kapama,Alfred Yonah, ambapo kwa kushirikiana na wanamuziki mbalimbali pia kama wadau wamekua wakiuinua muziki wa injili kwa kutoa mafunzo kwa wanamuziki kila siku ya Jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa sita mchana hapo hapo Sinza Kumekucha jijini Dar es Salaam.
kwa sasa muitikio wa watu umekua mkubwa sana na mafunzo yamekua yakitolewa kwa ada nafuu ya kuchangia uendeshwaji wa chuo hicho ambacho kimekua na maono ya kumuinua Mungu kwa njia ya kuwafundisha watu namna ya kumsifu Mungu kwa Vyombo vya Muziki na Sauti zilizopangwa kwa Ustadi na weledi.
Katika Kuelekea Mwishoni mwa mwaka huu wa 2015,Chuo hicho kipo katika maandalizi ya kufanya Event kubwa ya Muziki utakaopigwa Live katika Tamasha lililopewa jina "Christmass Jazz Night ambapo inatarajiwa kufanyika December 23, Mwaka huu 2015.
Sehemu ya maandalizi na mazoezi ni kama inavyoonekana katika picha hapa chini
Mwanamuziki Daniel Mfwango ,moja ya waalimu katika chuo hicho cha Muziki |