Msichana wa umri wa miezi 14 aliyenusurika ajali ya ndege mjini Juba, Sudan Kusini Jumatano amepata fahamu, madaktari wamesema
Msichana huyo anapokea matibabu katika hospitali kuu mjini Juba na ameweza kuwatambua jamaa zake, mwandishi wa habari wa Eye Radio ya Juba Philip Mabior amesema.
Watu 36 walifariki baada ya ndege hiyo ya kubeba mizigo kuanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Juba.
Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika lakini watengenezaji wa ndege hiyo wanasema ndege hiyo ilikuwa katika hali mbaya haikufaa kupaa.
Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa wametuma wapiga mbizi katika mto wa White Nile ktafuta miili, na kijisanduku cha kunakili maelezo kuhusu safari za ndege.
Ndege hiyo aina ya Antonov An-12, iliyokuwa ikitumiwa na shirika la Allied Services Limited ilikuwa safarini kuelekea Paloch, jimbo la Upper Nile, ilipoanguka karibu kilomita moja kutoka uwanja wa ndege kwenye ukingo wa mto Nile.
Haijabainika hasa iwapo msichana huyo ndiye pekee aliyenusurika ajali hiyo.
Alikuwa miongoni mwa watu wawili walioondolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege hiyo Jumatano, na ripoti baadaye zilisema mtu huyo wa pili alifariki baadaye.
Lakini mwanahabari Philip Mabior anasema kuna mtu wingine aliyenusurika ajali hiyo na anatibiwa katika hospitali hiyo.