Ikiwa ni muendelezo wa matukio yanayojiri nchini Tanzania yakihusisha ziara ya Mhubiri maarufu duniani toka nchini Nigeria T.B Joshua wa Kanisa la Synagogue Church of All Nations SCOAN, Alhamisi hii November 5, 2015 Nabii huyo amekua na muda mzuri na aliyekua mgombea uraisi kwa mwamvuli wa UKAWA na Waziri mkuu wa zamani wa Tanzania Mh.Edward Lowassa ambapo imeelezwa kwamba wamefanya naye Ibada maalum ya pamoja nyumbani kwa Mh.Edward Lowassa Ibada ambayo pia imehudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki wa Mh.Edward Lowassa
Katika Mitandao ya kijamii jioni hii picha zimesambaa zikimwonesha Nabii T.B Joshua akiwa na Mh.Edward Lowassa nje ya Bustani mara tu baada ya kumaliza Ibada hiyo nyumbani kwake mbunge huyo wa zamani wa Monduli na Waziri mkuu wa zamani wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Nabii T.B Joshua akiwa na Mh.Edward Lowassa nyumbani kwake mara tu baada ya kumaliza Ibada |
Katika Mitandao ya kijamii jioni hii picha zimesambaa zikimwonesha Nabii T.B Joshua akiwa na Mh.Edward Lowassa nje ya Bustani mara tu baada ya kumaliza Ibada hiyo nyumbani kwake mbunge huyo wa zamani wa Monduli na Waziri mkuu wa zamani wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Nabii T.B Joshua toka SCOAN akiwa na Mh,Edward Lowassa |