Baada ya makundi tofauti tofauti kuanza kujitokeza na kumtembelea nyumbani kwake Mbunge wa Monduli na Waziri mkuu wa zamani Mh.Edward Ngoyai Lowasa wakiwa na kauli mbiu ya kumtaka muda ukifika achukue form na kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2015,Hatimaye Kundi la Wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste kutoka mikoa tofauti tofauti nalo limejitokeza na kwenda Nyumbani kwa Mbunge huyo mjini Dodoma eneo la Area D na kumfanyia Maombi huku likimtaka muda ukifika basi agombee Urais na wao kama wachungaji watampa sapoti.