Wagombea tisa wakiwemo mdogo wa marehemu Deo Filikunjombe na mchekeshaji maarufu Emanuel Mgaya ama Masanja Mkandamizaji wamejitosa kuwania ubunge wa jimbo la Ludewa, mkoani Njombe kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Uchaguzi wa kumpata mbunge wa jimbo hilo ulilazimika kuahirishwa baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mbunge na mgombea wa jimbo hilo kupitia CCM, Deogratius Filikunjombe.
Miongoni mwa waliojitokeza kwenye kinyang’anyiro hicho ndani ya CCM ni mdogo wa marehemu, Philipo Filikunjombe na msanii wa vichekesho na muimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la ‘Masanja Mkandamizaji’.
Mh.Deo Filikunjombe alifariki Dunia October 15, kwa ajali ya Helikopta kwenye Hifadhi ya Selou eneo la Kilombero mkoani Morogoro ,Ikiwa ni siku 10 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Tanzania.
Mbali na Filikunjombe,Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na rubani wa helicopter hiyo Kapteni William Silaa,Blanka Haule na Egdi Nkwela.
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa,Luciano Mbosa amewataja wagombea wengine kua ni pamoja na Johnson Mgimba,James Mgaya,Zefania Jwaula,Deo Ngalawa,Dk.Evaristo Mtitu, na Simon Ngatunga
amebainisha kwamba tayari wagombea hao wamesha chukua fomu za kuwania ubunge jimboni hapo ndani ya chama hicho na sasa wanasubiri muda ufike wa kura za maoni ili waweze kuchujwa na kumpitisha mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya chama cha CCM katika uchaguzi huo utakaorudiwa kwenye jimbo hilo la Ludewa