Viongozi wa umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA wamekua ni miongoni mwa viongozi wa kitaifa nchini Tanzania ambao wamepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo maalum na Mhubiri wa kimataifa toka nchini Nigeria ,T.B Joshua ambaye yupo nchini Tanzania kwa ziara maalumu ikiwa ni pamoja na kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais wa awamu ya tano nchini Tanzania,Mh.John Pombe Magufuli,
Awali baada ya kuwasili nchini Tanzania,Nabii T.B Joshua alikutana na rais Jakaya Kikwete, na baadaye akakutana na Rais Mteule John Magufuli kisha akaelekea nyumbani kwa aliyekua mgombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwamvuli wa umoja wa vyama vinavyounda UKAWA Mh.Edward Lowassa,na kufanya naye mazungumzo kwa masaa kazaa.
katika mitandao ya kijamii baadhi ya picha zimeendelea kuongezeka kusambaa na sasa ni picha zinazomuonesha kiongozi huyo maarufu duniani wa Kiroho akiwa na mazungumzo na Mwenyekiti wa UKAWA Mh.Freeman Aikael Mbowe na Mh.Edward Lowassa.
kaa karibu nasi kwa kufungua blog hii kwa habari na picha zinazotufikia nasi tutaziweka kwa blog hii punde tu zinapotufikia.
T.B Joshua akiwa na viongozi waandamizi wa UKAWA,kutoka kushoto ni Mzee Kingunge Ngombare Mwiru,Mh,Edward Ngoyai Lowassa,Mh,Freeman Aikael Mbowe, T.B Joshua na Mwisho ni Mh.James Mbatia |
Nabii T.B Joshua akiwa katika mazungumzo na Mh.Edward Lowassa na Mh.James Mbatia ambao ni Viongozi wa UKAWA |
T.B Joshua akiwa na Mh.Freeman Mbowe na Mh.Edward Lowassa katika muendelezo wa mazungumzo |