Baada ya takriban miaka 48 ya kuvunjika kwa Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya nchi ya Tanzania na Israel hatimaye,Uhusiano huo umerejea upya na balozi mpya wa Israel nchini Tanzania amekwisha wasili na kwenda kujitambulisha ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kama utaratibu wa kidiplomasia unavyoelekeza,tayari kwa Ubalozi wa Israel kuanza kazi hapa nchini.
Awali taarifa rasmi toka kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ilitoa taarifa kwa uma kama inavyosomeka hapa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumatano Oktoba 28, 2015; amepokea Hati za Utambulisho za mabalozi wanne ambazo wataziwakilisha nchi zao katika Tanzania.
Katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amepokea Hati za Utambulisho za Mheshimiwa Balozi Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf wa Misri, Mheshimiwa Balozi Yahel Vilan wa Israel, Mheshimiwa Balozi Bayani V. Mangibin wa Philippines na Mheshimiwa Balozi Tan Puay Hiang wa Singapore.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Oktoba, 2015
Wachambuzi wa Mambo kwa nyakati tofauti wamekua na maoni tofauti tofauti kuhusua suala la Uwepo wa Ubalozi wa Israel nchini Tanzania
Baadhi wamekuwa wakisema kwamba Uwepo wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Taifa la Israel kwa namna moja ama nyingine ni kufungua Milango ya baraka kwa taifa kama Tanzania ambapo wamehusianisha kwa kutumia maandiko matakatifu kwa aya zinazosema "Atakayembariki Israel Atabarikiwa na Atakayemlaani Israel atalaaniwa na Mungu"
baadhi ya maoni ya watu mbalimbali katika mtandao ni kama ifuatavyo
Mchangiaji mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema kwamba
"kipindi fulani wakati wa utawala wa nyerere israel ilishambulia wapalestina sana na kuua watu wengi, sasa kwa vile nyerere alikua hapendi ukandamizaji alivunja uhusiano na israel kama ishara ya kupinga vitendo vyao dhidi ya wapalestina!
Kabla ya hapo uhusiano ulikua safi sana, wao ndio waliojenga majengo ya maana ya zamani hapa dar es salaam kama kitega uchumi, jengo la ushirika, chuo kikuu cha dar es salaam na hospitali ya bugando mwanza,sina uhakika na muhimbili ila nadhani ndio wenyewe! na ubalozi wao ulikua pale ubalozi wa marekani uliolipuliwa na magaidi
Maoni mengine ni kutoka kwa Kiongozi wa kanisa la BCIC Askofu Sylvester Gamanywa ambaye naye alikua na haya ya kusema kabla ya Ujio wa balozi huyu mpya wa Israel
"Tanzania haiwezi kufanikiwa kiuchumi na
kisiasa sababu haina mahusiano mazuri na Israel. Mataifa makubwa
yote duniani yana mahusiano mazuri na Israel kiuchumi.
Hii ikiwa ni pamoja na Marekani, China, Japan, India, Ujerumani, Urusi, Brazil, Uingereza, Ufaransa na Italia; lakini Tanzania haina hata balozi israel. 2% ya wamarekani ni wayahudi.
Akatoa ujumbe kwa serikali ya Tanzania kufungua mahusiano na Israel amebainisha zaidi kwa kusema kwamba "Tuache kuingilia ugomvi wa Ishmael na Isaka sisi hautuhusu
Askofu Gamanywa alisema tukiwa connected na Isaka, baraka za kiuchumi zitakuja.
Gamanywa anasema "pigeni kelele na Israel lakini pataneni na Israel kiuchumi kama mataifa mengine ili Tanzania ifanikiwe.
Alibainisha zaid kwa kusema "Ishmail ni mwarabu na Isaka ndipo baraka zetu zilipo kutokana na mandiko katika biblia. Sisi ugomvi wa waarabu na wayahudi hautuhusu.
Tunachotakiwa ni kuinuka kiuchumi na hiyo haiwezekani bila kuwa na mahusiano mazuri na Israel. Waisrael wameahidiwa kuwa kichwa na sio mkia katika biashara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Balozi mpya wa Israel hapa nchini mwenye Makazi yake nchini Kenya, Mhe. Yahel Vilan mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho. Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2015. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumatano Oktoba 28, 2015; amepokea Hati za Utambulisho za mabalozi wanne ambazo wataziwakilisha nchi zao katika Tanzania.
Katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amepokea Hati za Utambulisho za Mheshimiwa Balozi Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf wa Misri, Mheshimiwa Balozi Yahel Vilan wa Israel, Mheshimiwa Balozi Bayani V. Mangibin wa Philippines na Mheshimiwa Balozi Tan Puay Hiang wa Singapore.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Oktoba, 2015
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Vilan, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula. |
Balozi Vilan akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Elibariki Maleko |
Balozi Vilan akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga |