Nabii na Mhubiri wa Kimataifa toka nchini Nigeria na kiongozi wa kanisa la Synagogue Church of All Nation SCOAN Temitope Balogun Joshua maarufu kama T.B Joshua amewasili nchini Tanzania Jana tarehe 3November 2015,ikiwa ni ziara maalumu kushiriki na kuhudhuria katika sherehe za kuapishwa kwa rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania zinazotarajiwa kufanyika siku ya Alhamis tarehe 5November 2015.
|
Prophet T.B.Joshua akiwa na Rais Mteule wa Tanzania,John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili nchini Tanzania |
|
Baada ya kuwasili nchini, Nabii T.B Joshua alipokelewa air pot na mwenyeji wake yani rais mteule wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli na kuelekea moja kwa moja Ikulu kukutana na rais anayemaliza muda wake,Jakaya Mrisho Kikwete na kufanya nae Mazungumzo,
|
Prophet T.B Joshua akiwa na mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili nchini Tanzania |
|
T.B Joshua na Rais Jakaya Kikwete |
Katika Uwepo wake hapa nchini T.B Joshua amefanya mazungumzo na Familia ya rais mteule John Magufuli
|
T.B Joshua akiwa na familia ya rais Mteule John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam |
na baadae pia akakutana na aliyekua waziri mkuu wa zamani na aliyekua mgombea urais kupitia CHADEMA,na umoja wa vyama vinavyounda UKAWA Mh.Edward Lowassa na familia yake na kufanya nao mazungumzo pia.
|
T.B Joshua akiwa na Mh.Edward Lowassa na Familia yake jijini Dar es Salaam |
T.B.Joshua anatarajiwa kushiriki pia katika zoezi la kuapishwa kwa rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli zinazotarajiwa kufanyika uwanja wa taifa siku ya Alhamisi tarehe 5,mwaka huu 2015.
|
T.B Joshua akiwa na Mh.Edward Lowassa |