Kanisa la Mwanza International Community Church jijini Mwanza chini ya Uongozi wa Mchungaji Zakayo Nzogere wameendelea na hatua nyingine zaidi za ujenzi wa jengo hilo bora na la kisasa la kuabudia,ambapo litakua na uwezo wa kuchukua watu wengi zaidi katika Ibada na kumwabudu Mungu katika mazingira mazuri na ya kupendeza ndani ya jiji la Mwanza.
Katika ukurasa wa facebook wa Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo la MICC ,Zakayo Nzogere blog hii imemnukuu na hiki ndicho alichokisema,
WEKA ALAMA KATIKA JENGO HILI: Kazi ya ujenzi wa kanisa la MICC Jijini
Mwanza inaendelea vizuri. Weka alama katika jengo hili kwa kununua japo
bati 1 @ 45,000/=.Tayari varanda imesha ezekwa. Ndani tumeaanza kumwaga
jamvi na kujenga madhabahu. Lengo letu ni kuezeka jengo zima kabla ya
mwisho wa November. Nashukuru sana kwa maombi na mchango wako.
Baadhi ya picha zinazoonesha namna ujenzi wa jengo hilo la kuabudia la MICC ni kama zinavyoonekana hapa
Waweza kusapoti huduma hii kwa kulike page ya kanisa la MICC na kisha fuata maelekezo namna ya kushiriki baraka hii kwa mchango wako bofya hapa MICC Facebook Page