Kutoka Nchini Kenya Mwanamke mmoja mwenye Umri wa miaka 70 ameibua kali ya mwaka baada ya kufanya harusi kwa imani na kutangaza kwamba anaolewa na Yesu,mwanamke huyo aliyesema kwamba ameolewa na Yesu amesema kwamba ,uamuzi wake ulitokana na sababu kwamba kuwa umri aliofikisha haungemwezesha kupata mume mwingine hapa ulimwenguni.
Bi Josephine Wangui Njoroge, mwenye umri wa miaka 70, alifanya harusi iliyohudhuriwa na halaiki ya watu, katika Kanisa la African Independent Pentecostal Church of Kenya (AIPCK), lililo Kamirithu, Limuru, Kaunti ya Kiambu.
Tazama Video yake hapa
Mwanamke huyo aliyekuwa ameolewa kwa njia ya kitamaduni katika mwaka wa 1963 alifiwa na mumewe katika mwaka wa 1982, ambaye pamoja walikuwa wamejaliwa watoto 10.
“Bwana wa ulimwengu aliniacha. Hakuniambia twende naye. Sasa huyu ambaye aliniachia ananifurahisha ndio maana niliona heri niolewe naye,” akasema Bi Njoroge, kwenye mahojiano ya kipekee na Taifa Leo, nyumbani kwake Limuru.
Watu waliofika kushuhudia harusi hiyo walitamani kumwona Yesu akifunga ndoa, lakini wachungaji wa kanisa hilo ndio walijitwika jukumu la kumvika pete Bi Njoroge.
“Hakuna bwana wa ulimwengu atanioa ndio maana niliamua niolewe na Yesu. Ukizingatia wale watoto niko nao, singekubali niolewe na mume mwingine. Watoto wangu ni wakubwa. Yesu ndiye bwanangu. Ananifanyia matendo mazuri na ananilinda,” akasema. Kulingana naye, maisha yake yameweza kuwa yenye furaha nyingi na hata matatizo huwa hayambabaishi kutokana na imani yake kuwa ana mume anayeweza kufanikisha mahitaji yake yote
Umri mkubwa
Furaha yake inadhihirika na jinsi alivyo mchangamfu na mwenye nguvu licha ya umri wake mkubwa.
Alisema alikuwa ametamani sana kufanya harusi na azimio lake lilifanikishwa kwa njia ya kipekee.
“Kama bwanangu angekuwepo tungefanya harusi naye. Wakati bwanangu aliaga roho yangu ilitamani nifanye harusi wakati mmoja,” akasema.
Familia yake inafurahia sana uamuzi aliofanya na wanasema Yesu ndiye amekuwa baba yao tangu baba mzazi aage dunia miaka 33 iliyopita.
Mwanawe wa nne, Bw Geoffrey Mwaura Njoroge, alisema sasa wanatarajia kuwa na maisha bora zaidi.
“Mama ametulea katika mambo ya kiroho. Ametufundisha tukimlilia huyu bwana na kupeleka mahitaji yetu kwake atatutimizia.
“Tumeona huyo bwana ni mzuri kwa hivyo wakati mama aliamua kuolewa naye, tukasema sasa yeye atakuwa akitutendea zaidi ya jinsi alivyokuwa akitutendea,” akasema.
Ingawa tukio hili huenda likaonekana kuwa la kushangaza na wengi, kanisa hilo linasisitiza hakuna chochote kisicho cha kawaida.
Shemasi Mkuu wa kanisa la AIPCK, Kamirithu Bw Paul Njenga, alisema kumekuwepo wanawake watano waliofunganishwa ndoa na Yesu nchini katika matawi mengine ya kanisa hilo nchini.
Kulingana naye, kanisa hilo lina matawi yapatayo 1,000 nchini na limekuwepo kwa zaidi ya miaka 50.
“Katika kanisa letu huwa tunaruhusu harusi aina hiyo. Kile hatukubali ni ndoa ya mume kwa mume au mke kwa mke, lakini ndoa ambayo ni ya mtu anayetaka kujitolea kuishi ndani ya Mungu bila mambo mengine, hiyo tunakubali,” akasema.
Alieleza kuwa harusi hiyo hufanywa kama ishara ya kuonyesha kuwa mtu amejitolea kikamilifu kumtumikia Mungu, na hata wanaume wanaruhusiwa 'kufunga ndoa’ na Yesu.
“Kama mtu amejitolea kabisa kumtumikia Mungu anaweza kufunganishwa ndoa...si eti yesu atakuwa amesimama kando bali ni kuwa hana jambo lingine isipokuwa kumtumikia Mungu siku zote maishani mwake,” akasema.
Ukitaka kufanyiwa harusi aina hii, Bw Njenga alisema utahitaji kuwa mjane mwenye umri wa miaka 65, vile amelea watoto wake, na majirani kutoa ushuhuda kumhusu.
Kulingana naye, umri huo umetokana na maandiko katika kitabu cha Timotheo wa kwanza, mstari wa tano kwenye Biblia Takatifu.
Source: swahilihub Kenya