Mkazi mmoja wa Lusaka nchini Zambia ambaye wiki mbili zilizopita alijikuta akipoteza mguu wake mmoja baada ya kupata ajali,siku chache kabla ya harusi yake,hatimaye amefanikisha azma yake baada ya kufunga ndoa na mchumba wake huyohuyo huku yeye akiwa amelazwa kitandani katika Hospitali moja nchini humo
Suzyo Muzuri mwenye umri wa miaka 28 amefunga ndoa hiyo na bi Diniwe Bowa mwenye umri wa miaka 27 katika harusi iliyofanywa chini ya Askofu Andrew Mwenda wa kanisa la Bethel Christian Center harusi iliyofanyika ndani ya wodi namba 11 ya Hospitali iliyopo ndani ya chuo kikuu UTH.
Sherehe hiyo ya ndoa imehudhuriwa na ndugu jamaa na wanafamilia wa familia za bwana na bibi harusi ambao walisimama kushuhudia wawili hao waliopendana wakifunga ndoa yao na kuanza maisha mapya kama mume na mke
Hayo ndiyo yaliyojiri huko Lusaka,Nasi tunawatakia maisha mema na yenye baraka tele katika ndoa yao maharusi hawa ambao wameonesha Upendo kwa Vitendo na sio kwa maneno tuu