Mh.Freeman Mbowe Aizindua rasmi DVD Album ya Flora Mbasha pamoja na Bendi
byAdmin-
0
Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Tanzania,Flora Mbasha mwisho wa wiki hii amefanikiwa kufanya uzinduzi wa album yake mpya kabisa na pia kuzindua Bendi ya muziki ambayo ataanza kufanya nayo huduma za kimuziki wa injili kuanzia sasa.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo alikua ni mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Aiakel Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Same mkoani Kilimanjaro.
Uzinduzi huo uliambatana na burudani ya nyimbo za injili kutoka kwa wanamuziki mbalimbali ambao waliambatana na Flora mbasha katika kuiweka wakfu DVD yake mpya pamoja na Bendi,Miongoni mwa wanamuziki walihudhuria uzinduzi huo ni pamoja na Ambwene Mwasongwe, Upendo Nkonne, Joseph Nyuki, Christopher Mwahangila, Christina Matai, Neema Gasper, na Furaha Isaya.
Video na Picha za Uzinduzi huo ni kama zinavyoonekana hapa chini kama zilivyopigwa na Uncle Jimmy ambaye alikuwepo eneo la tukio
Mh.Freeman Mbowe akizungumza jambo wakati akizundua Album hiyo
Mwanamuziki Flora Mbasha akiwa VIP Hall kabla ya kuingia Ukumbini
Back Vocal au waimbaji wa bendi hiyo ya Flora Mbasha wakijiweka sawa kabla ya kuingia ukumbini
Flora Mbasha
Mwanamuziki Ambele Mwasongwe akiperfom katika Uzinduzi huo
Mh,Freeman Mbowe
Mh.Freeman Mbowe akiwa na ujumbe wake wakiingia Ukumbini huku ulinzi ukiwa umeimarishwa
Mh,Freeman Mbowe akiwa na ujumbe wake ndani wakiwa meza kuu kama mgeni Rasmi katika uzinduzi huo
Mh,Freeman Mbowe akiizindua DVD album yake Flora Mbasha