Polisi katika Jimbo la Carolina Kusini nchini Marekani wamesema mtu mmoja aliyekuwa na bunduki amewapiga risasi na kuwaua watu tisa ndani ya kanisa la Methodist lililoko eneo la Charleston.
Wamesema kwa sasa wanamtafuta mshukiwa huyo anayeaminiwa kuwa kijana wa Kizungu mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka ishirini.
Shambulio hilo limefanyika ndani ya kanisa la Emmanuel African Methodist Church maarufu kama AME, kanisa linaloaminika kuwa la zamani zaidi linalotumiwa na watu wa asili ya Afrika nchini Marekani.
Polisi wamesema kuwa shambulio hilo linatokana na chuki ya ubaguzi wa rangi ambapo pia limehusishwa na nguvu ya kisiasa kati ya vyama viwili vya siasa katika eneo la Charleston huko South Carolina kutokana na kile kinachodaiwa kuwa limefanyika saa chache kabla ya Mchungaji Pinckney kukutana na mwendesha kampeni wa Chama cha Democratic cha Marekani, Hillary Clinton, katika sehemu ya kampeni ya kuwania urais wa nchi hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo alimtaka mama mmoja wa makamu kuondoka kanisani hapo kabla hajatekeleza azma yake hiyo ya kufanya shambulio hilo.
Lengo la kumwondoa mama huyo lilikuwa ni kumfanya aende akawaambie watu wengine kilichotokea.
Watu wanane walikufa papo hapo na mwingine alifariki akiwa anapata matibabu hosipitali. Aidha majeruhi mmoja anayeendelea kupata matibabu ameripotiwa kuwa katika hali nzuri.
Mchungaji Pinckney wa kanisa hilo na Seneta wa Jimbo la Carolina Kusini, ni miongoni mwa walioripotiwa kuuawa kutokana na shambulio.
Duru za habari kutoka kwa walioshuhudia tukio hilo zinasema mtoto wa miaka mitano amenusurika kifo kutokana na shambulio hilo baada ya kuambiwa na bibi yake aliyeambatana naye kanisani kuwa asali kabisa maana hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya uhai wao.
Hali ya sintofahamu ikiwa imetanda kwenye eneo lilipotokea shambulio |
Shambulio hilo limefanyika ndani ya kanisa la Emmanuel African Methodist Church maarufu kama AME, kanisa linaloaminika kuwa la zamani zaidi linalotumiwa na watu wa asili ya Afrika nchini Marekani.
Askari wakiwa katika harakati za kuimarisha ulinzi eneo la tukio. |
Barabara zikifungwa. |
Waumini wa kanisa la AME na watu wa majirani wa eneo la tukio wakiwa katika majonzi baada ya kutokea shambulio hilo. |
Watu wanane walikufa papo hapo na mwingine alifariki akiwa anapata matibabu hosipitali. Aidha majeruhi mmoja anayeendelea kupata matibabu ameripotiwa kuwa katika hali nzuri.
Mchungaji Clementa Pinckney aliyeripotiwa kuuawa kutokana na shambulio hilo. |