Hatimaye ratiba kuhusu maazishi ya aliyekuwa askofu mkuu wa makanisa ya Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Moses Kulola, imetoka na inaonyesha kuwa maazishi yatafanyika Mwanza siku ya Jumatano Septemba 4 kwenye kanisa la EAGT Bugando.
Akitoa taarifa hiyo eneo ambapo msiba umewekwa, EAGT Temeke, katibu wa EAGT kanda ya Mashariki Kusini, Askofu Alphonse Mwanjala ameeleza kuwa kutakuwa na ibada za maombolezo hadi Ijumaa na kwa siku ya Jumamosi mwili utawasili Temeke kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa mchana ambapo utaagwa na hatimaye kupelekwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nyerere kwa ajili ya kuusafirisha siku ya Jumapili kuelekea Mwanza.
Na huko Mwanza pia taratibu nyingine zitafanyika na hatimaye mwili kupumzishwa siku ya Jumatano EAGT Bugando.
Christ Gospel Messengers watakuwepo Temeke na kufanya mkesha kwa siku zote hadi mwili utakaposafirishwa.
Kwa upande mwingine Katibu Mkuu wa baraza la makanisa ya Kipentekoste (PCT) nchini, Askofu David Mwasota, anasikitika kutangaza kifo hicho na kuwataka wachungaji, maaskofu, mitume, manabii na walimu wote kukutana siku ya kesho kwanye kanisa la mito ya Baraka kwa Askofu Bruno Mwakibolwa ili kufanikisha zoezi zima la kumpumzisha Askofu Kulola atakesafirishwa kwenda Mwanza.
Katika mahojiano na Gospel Kitaa, Askofu Mwasota ambaye pia ni mtoto wa kiroho wa Askofu Kulola, amesema kuwa ni vema viongozi wa makanisa wakajitokeza ili kufanikisha zoezi la Mzee Kulola ambaye ametumiwa na Mungu kwa namna ua kipekee katika kueneza injili kwa mataifa yote.