kupitia kipindi hiki Vijana wa kitanzania wasio na Ajira watapata nafasi ya kuona Vijana wa Kitanzania wakichambua na kuonesha namna wanavyopambana na tatizo Sugu la Ajira nchini Tanzania,,,
Pia watanzania watapata nafasi ya kuona na kufahamu kuhusu watu maarufu na wasio maarufu kuhusu mafanikio yao hivi leo lakini pia watajua safari zao kimaisha na Nyakati zao Ngumu zilikuaje awali,walipopita na safari yao kwenye kuukataa Umaskini kutoka Point A mpaka walipo leo hiii yani From Zero to Hero,,,,,
Miongoni mwa watu hao maarufu ikiwa ni pamoja na MC Pilipili, Swebe, Mrisho Mpoto,Rashid Matumla na wengine wengi...
watazamaji pia watapata darasa la Bureee la Ujasirimali kwa kutazama kipindi hiki maelezo yatakayokua yanatolewa na wataalamu na walimu mbalimbali waliobobea na wanasaikolojia katika Harakati hizi za kuutafuta mwarobaini wa Tatizo la Ajira nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na MC Anthony Luvanda,James Mwang'amba, Samuel Sasali, Sethi Katende na mwana saikolojia Chriss Mauki.
kwa mujibu wa Mtayarishaji wa kipindi hicho Baraka Samson ameeleza kwamba ""Sisi tumeanza kwa Kujenga Jukwaa la Majobless nchini kutoa ya Moyoni,,,,dhidi ya Kila Kinachosababisha Bomu hili linalosubiri muda tuu Kulipuka tunategemea wadau wengine toka sekta mbalimbali kutupa sapoti ili mwisho wa siku tuweze kuondoa ama hata kupunguza tatizo la ajira nchini Tanzania na kutoa elimu na mbinu za kuwapunguzia makali ya maisha vijana wengi wa kitanzania ambao wanataabika mitaani kwa kukosa ajira""
Kipindi hicho kitakua kikiendeshwa na mtangazaji Mrisho Mbogolume mbaye awali aliwahi kutangaza katika kituo cha Radio Free Africa cha jijini Mwanza.
Unaweza kutazama kionjo cha Kipindi hiki kupitia video hii