Kutoka kwenye Moja ya account za mitandao ya kijamii zinazoendeshwa na huduma ya T.B Joshua zimewekwa Picha zinazomuonesha nabii Temitope Balogun Joshua au maarufu kama T.B. Joshua ambaye alizaliwa June 12, 1963 nchini Nigeria na amekua kiongozi wa kanisa kubwa nchini Nigeria lijulikanalo kama The Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) ambapo kanisa hilo pia linaendesha kituo cha televisheni chan Emmannuel TV
Nabii T.B Joshua ametokea kujitwalia umaarufu sana katika
nchi nyingi za Afrika na barani Ulaya na Asia kwa kutabiri mambo
mbalimbali ambayo baadae yalikua yakitokea kweli na kuripotiwa na vyombo
mbalimbali vikubwa na vinavyoheshimika Duniani.
|
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 17 |
Nabii T.B.Joshua amewahi kutunukiwa Nishani kama Officer
of the Order of the Federal Republic (OFR) kutoka kwa serikali ya
Nigeri mwaka 2008 na pia aliwahi kuchaguliwa kua mtu wa Karne toka
kabila la Yoruba nchini Nigeria ambapo alipewa wadhifa huo toka taasisi
ijulikanayo kama Pan-Yoruba media outlet Irohin-Odua
|
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 20 |
Nabii T.B. Joshua pia amewahi kutambulika kama moja ya
watu 50 toka Afrika wenye nguvu ya Ushawishi kwa jamii wadhifa aliopewa
na taasis ya Pan-African magazines na pia kumtaja kama moja ya watu
maarufu sana Duniani
|
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 25 |
Amejulikana sana duniani kupitia mitandao ya kijamiii ambapo T.B. Joshua anatajwa kua na mashabiki wapatao Milion 1,na laki 5 kupitia akaunt ya Facebook na mamia ya video zake zilizopo kwenye mtandao wa Youtube baadhi ziliwahi kuleta utata sana duniani kutokana na utata wa mambo aliyowahi kutabiri na hatimaye kusababisha mamilion ya watu duniani kuzitafuta hizo video ili wazitazame kwenye mtandao.
Jarida maarufu la FORBES mwaka 2011 lilimtaja nabii T.B. Joshua kua anashikilia nafasi ya tatu katika wachungaji matajiri zaidi nchini Nigeria akiwa na utajiri unakadiriwa kufikia Dola za kimarekani Milion 10 mpaka 15 (US$ 10-15 million )
endelea kutembelea blog mara kwa mara kazi yangu ni kuhakikisha unahabarika na kupata taarifa mbalimbali kadri zinaponifikia