Mchungaji aliyewalisha nyasi wafuasi wake sasa awanywesha petroli akiwahadaa kuwa itabadilika na kuwa maji ya nanasi.
Mchungaji Lesego Daniel ameibua utata nchini Afrika Kusini baada ya kuwataka wafuasi wake kunywa petroli huku akiwaahidi kuwa petroli ile ingebadilika na kuwa maji ya nanasi.
Video ya tukio hili ni kama inavyoonekana hapa chini
Mchungaji Lesego Daniel ameibua utata nchini Afrika Kusini baada ya kuwataka wafuasi wake kunywa petroli huku akiwaahidi kuwa petroli ile ingebadilika na kuwa maji ya nanasi.
Mchungaji huyo alipata umaarufu mapema mwaka huu alipowataka wafuasi wake kula nyasi ili wawe karibu na Mwenyezi Mungu.
Viongozi wa kidini nchini Afrika Kusini walimkashifu vikali mchungaji huyo huku wakisema kuwa mchungaji huyo alikuwa akihatarisha maisha ya wafuasi wake ili kujipatia umaarufu wa haraka.
Profesa wa theolojia Fika Janse van Rensburg kutoka chuo kikuu cha Northwest alisema, "Katika mafundisho ya kikristo, Mwili ni hekalu la Mungu na kwa kunywa petroli unaidhuru mwili."
Mchungaji Daniel aliyepata umaarufu baada ya video yake, iliyoonyesha akiwaamuru wafuasi wake kula nyasi, kusambaa kwenye mtandao wa intaneti.
Mapema mwezi huu raia 84 wa Afrika Kusini walifariki katika kanisa la mchungaji T.B Joshua baada ya jengo hilo kuporomoka. Wafuasi hao wanadaiwa kumfuata mchungaji Joshua kwa imani kuwa anaweza kuponya magonjwa kama ukimwi na saratani.