Hatimaye Mahakama ya Rufaa ya wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza imemrudishia haki yake Bi Elizabeth Kulola Mama mjane wa Marehemu askofu Moses Kulola ,aliyekua Askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania EAGT,na kumkabidhi haki ya kusimamia Mirathi hiyo ya marehemu tofauti na Hukumu iliyotolewa hapo awali na mahakama iliyokua imempa haki hiyo Mchungaji wa kanisa la City Center la jijini Dar es Salaam mchungaji Florian Katunzi kua msimamizi wa mirathi ya marehemu Askofu Moses Kulola.
|
Bi Elizabeth Kulola Mama mjane wa Marehemu askofu Moses Kulola |
Akiongea na Blogu hii mmoja wa watoto wa Marehemu Askofu Moses Kulola, bwana Abel Kulola ameelezea kufurahishwa na hukumu hiyo na kuelezea kua hatimaye mahakama imewatendea haki wao kama familia ya marehemu na hata kwa mama yao ambaye alikua kila kukicha akishinda na machozi ya huzuni baada ya hukumu ya kwanza iliyotolewa na mahakama ya mwanzo iliyoonekana kuwanyang'anya haki yao kama ndugu wa marehemu na kumpa haki hiyo mtu wa nje ya familia yao.
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokua akimfariji Bi Elizabeth Kulola kipindi cha msiba wa askofu Moses Kulola |
katika shauri hilo mahakama ya rufaa ilielezea kukiukwa kwa baadhi ya vifungu katika kesi hiyo ambapo kesi hiyo ambapo ilionekana awali ilisikilizwa kimakosa katika mahakama ya mwanzo kesi ambayo haikupaswa kusikilizwa na kutolewa hukumu katika mahakama hiyo.
Hata hivyo baada ya kuipitia kesi hiyo Mahakama ilitengua hukumu ya awali iliyokua imempa haki ya kusimamia mirathi yote ya marehemu Askofu Moses Kulola na kumpa haki hiyo Mama mjane wa Marehemu Bi Elizabeth Kulola,ambapo baada ya kupewa haki hiyo na mahaka hiyo ya rufaa mama huyu alishinda siku nzima akidondokwa na machozi ya furaha na kumshukuru Mungu kwa kujibu kiu na kilio chake cha muda mrefu tangu mgogoro huu wa mirathi ulipoanza na kutonesha kidonda cha msiba wa mume wake.
Askofu Moses Kulola ni moja ya wahubiri wakubwa sana duniani ambapo katika kipindi cha maisha yake duniani aliweza kuzunguka vijiji mikoa nchi na mataifa mengi sana duniani katika kuihubiri injili na kuwaelekeza watu wamwamini Mungu na kuishi maisha mema, lakini pia anakumbukwa kama baba wa Kiroho wa watumishi wachungaji na wainjilist wote hapa Tanzania.
|
Marehemu Askofu Moses Kulola |
lakini ikiwa ni mwaka mmoja tuu umepita tangu apumzike kwa Amani familia yake iliingia katika sintofahamu ambayo ilionekana kuivuruga familia hiyo baada ya kujitokeza mchungaji Florian Katunzi aliyeibuka na madai ya kuwa kipindi cha uhai wa marehemu yeye ndiye alipewa jukumu hilo na marehemu la kusimamia mirathi yote ya marehemu kipindi atakapokua ametwaliwa na Bwana.
|
Mchungaji Florian Katunzi wa kanisa la Dar es salaam City Center ,ambaye awali ndiye aliyekua amepewa na mahakam haki hiyo ya kusimamia Mirathi ya Marehemu Askofu Moses Kulola |
katika sintofahamu hiyo shauri hilo lilifika hadi mahakamani ambapo mlalamikaji katika kesi hiyo Mch.Katunzi alipeleka vielelezo vya kuonesha uthibitisho juu ya kupewa haki hiyo na marehemu na hatimaye mahakama ikatoa hukumu na kumpa ushindi mchl.Katunzi wa kusimamia mirathi ya marehemu Askofu Kulola.
|
Marehemu Askofu Moses Kulola akiwa na mwanae Mch.Dr.Daniel Moses Kulola akimkabidhi mikoba ya injili kuendeleza pale ambapo alishia. |
Hivi karibuni familia hiyo baada ya kutoridhishwa na hukumu hiyo iliyotolewa waliamua kukata rufaa na hatimaye siku ya ijumaa 19september 2014 katika mahakama ya rufaa ya wilaya ya nyamagana hukumu ikatolewa na kumtangaza Bi Elizabeth Kulola kua ndiye msimamizi Halali wa mirathi ya marehemu mume wake.
Unaweza kusoma habari za nyuma za mwendelezo wa kesi hii kama zilivyoripotiwa hapo awali na blog hii kwa kubofya hizi link.