Maudhui ya ujumbe humtambulisha aubebaye ujumbe
“Heri kusikiliza laumu ya mwenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu.” Mhubiri 7:5
Kanuni nyingine ya kimsingi ambayo huniongoza katika kufanya maamuzi yangu binafsi na hasa maamuzi yahusianayo na taarifa ni kanuni ya maudhui (content).
Haijalishi mtu fulani ni maarufu, mshuhuri kiasi gani au ana sura nzuri kiasi gani… Akili na ufahamu wangu huelekea kwenye maudhui kisha kutoka huko maamuzi hufanyika.
Sulemani, moja ya wenye hekima kuwahi kuishi duniani, anatutambulisha kwenye kanuni muhimu “Heri (ni baraka) kusikiliza laumu ya mwenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu.”
Wimbo wa wapumbavu kwa maana hizi:
* Wimbo huo humilikiwa na wapumbavu
* Wimbo huo ni maalumu kwaajili ya wapumbavu- watu waliokusudiwa kuguswa, waliolengwa (targeted audience) ni wapumbavu
* Maudhui yake/wanauzungumziwa ndani ya wimbo ni wapumbavu
Katika wigo mapana huo, wimbo wa wapumbavu haupaswi kusikilizwa! Nitarejea kujadili walau kwa uchache kuhusu jambo hilo.
Ni kama dhihaka fulani hivi mimi ninaona! Kwasababu kimsingi wimbo hasa muziki huwa na namna fulani ya kuiburudisha nafsi/akili na kwa upande
mwingine laumu huleta huzuni kwenye nafsi/moyo wa mtu na tena humfanya mtu asiwe katika hali ya kujisikia vizuri (unconfortable).
Usuli wa laumu ya mwenye haki si kumfanya mtu ahuzunike na akate tama bali ni kumrejesha kwenye mstari anaopaswa kutemebea mtu.
Haya ndiyo yamekuwa maisha ya mzee Kulola… amezunguka nchi zima ya Tanzania na nchi jirani kuleta huzuni na disconforts ndani ya mioyo ya watu wengi ili kuwafanya wawe watu bora zaidi ya walivyokuwa hapo awali.
Biashara yake kubwa ilikuwa ni kuhakikisha watu na taifa linapatanishwa na moyo wa Mungu! Amesimama kwenye majukwaa mengi na kuelezea LAUMU yake kwa mtu binafsi na taifa na kupitia laumu hiyo maisha ya watu yanadhihirisha mambadiliko!
Kwa wafuatiliaji wa muziki na masuala ya habari hapa kwetu Tanzania wanajua kuwa Baraza la sanaa na mamlaka husika za maadili huchambua Maudhui ya nyimbo na kuchukua hatua zinazostahiki.
Kuna wimbo kutoka kwa yule kijana maarufu mwimbaji ambao ulishawahi kuzuiliwa kupigwa redioni kutokana na maadhui yaujazayo wimbo husika.
Well, ni vigumu sana kuuelewa kama mtu hutambui ya kwamba taarifa ni chakula cha nafsi! Taarifa iliyo katika picha, maandishi, sauti n.k zote huelekea kwenye nafsi kupitia milango ya fahamu. Kwahiyo, nafsi za watu hula kutoka huko!!!
Baada ya kuwekeza muda wangu mwingi kutazama baadhi ya kazi za watu hawa watatu: Mzee Kulola, na wale vijana wawili na kuzichambua kwa umakini
kimaadili na kifalsafa ndipo nilipofikia Hitimisho na Ujasiri ya kwamba huyu mzee ni shujaa:
* Je, kazi ziliwafanya watu kuwa bora Kuliko hapo awali (ubora ni ule wa “ufanikiwe kama vile roho yako ifanikiwavyo” yaani Inside-Out).
* Je, kazi zao zimeongeza ubora kwenye taifa/makundi ya watu?
* Je, Maudhui ya kazi zao hayaachi tashwishwi mbele ya rika na makundi tofauti ndani ya jamii?
Asomaye na afahamu!
Hitimisho:
Ninaheshimu sana kazi na maisha mbalimbali ya watu wengi waliowahi kuishi hapa kwetu Tanzania. Pamoja na yote, sizuiliwi kuwa na msimamao wangu, hasa ninapoulizwa msimamo wangu juu ya mambo kadhaa ya kimaisha na kijamii.
Maisha huongozwa na kanuni na hizo ndiyo huzitumia kuweka misimamo na mitazamo yangu. Haijalishi mtu fulani ni wa dini kiasi gani, mzuri, maarufu, anapendwa na wengi n.k lakini wote wanapimwa kwa kipimo kilekile cha kanuni!
Hayo ni baadhi tu ya majibu yangu binafsi, Kwanini hata sasa ninamuona mzee Dr. Moses Kulola kwamba ni moja ya mashujaa kuwahi kutokea kwenye nchi ya Tanzania.
Mithali 13:11
Uga wa Mkufunzi
“Darasa la kanuni za maisha”
Na James Kalekwa
www.mjapinc.blogspot.com
Kila siku ya Jumatano
“Heri kusikiliza laumu ya mwenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu.” Mhubiri 7:5
Mwandishi James Kalekwa |