Mwanamuziki mahiri wa nyimbo za injili toka nchini Afrika Kusini ajulikanaye kama Keke Jumapili hii ya Pasaka ameungana na wanamuziki mbalimbali toka Tanzania,Kenya,Zambia naUingereza katika kumsifu Mungu ndani ya Pasaka la Pasaka ambalo huandaliwa na Msama Promotion chini ya Alex Msama.
Katika Tamasha hilo mgeni rasmi alikua ni Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania mh.Bernad Membe ambaye alimuwakilisha rais Jakaya Kikwete kutokana na kutoweza kuhudhuria kwa kuwa nje ya nchi kwa shughuli za kiserikali.
Miongoni mwa wanamuziki walioperfom katika tamasha hilo ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Sara K kutoka Kenya, Glorious Worship Team, John Lisu, Mwanamuziki kutoka UK na Keke Kutoka South Africa pamoja na Rose Muhando.
Mhe. Benard Membe
akisikiliza risala kutoka kwa Mchungaji Mwasota ambaye ni Mwenyekiti wa
Makanisa ya Pentekoste Ukanda wa Dar-es-Salaam
|
Keke mwanamuziki kutoka Africa Ya Kusini akihudumu katika Uwanja wa Taifa
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Membe akiongea siku ya Jana kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya
|
Laura Msama Mke wa Msama akiwa amekunja goti wakati akisalimiana na Mhe. Membe |
Mhe. Membe akiwa anasalimiana na Keke |
Mwanamuziki kutoka Zambia Ephrahim Sekeleti akiwa anapasha pamoja na Backers Vocalists wake.
|
Upendo Kilahiro akiwa anaenda sawa katika Uwanja wa Taifa |
Mise Anaeli akuwa anapuliza tarumbeta Uwanjani |
Sarah K Mwanamuziki Kutoka Kenya akiwa anaimba Wimbo Wake "Liseme" |
"Kwani Ni Jambo Lipi hilo, Yeye asiloliweza"
|
Baadhi ya Waimbaji Wa Glorious Worship Team wakiwa Jukwaani wakienda sawa
|
Mwanamuziki Nguli kutoka Africa Ya Kusini Keke akiwa Jukwaani |
Backers Vocalists wakiwa wanaenda sawa |
Mpiga drums nambari moja wa Keke akiwa anaenda sawa |