Mabomu mawili yamelipuka , mapema wiki hii Jumatatu huko Zanzibar, ambapo mlipuko mmoja umelipuka karibu na kanisa la Anglican na mwingine ukilipuka kwenye mgahawa wa Mercury eneo ambalo hutembelewa sana na watalii kutoka nje ya nchi
Taarifa zimeeleza kua mpaka sasa hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa na milipuko hiyo licha Kamishna wa polisi msaidizi Mkadam Khamis kueleza kua Uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha milipuko hiyo na wahusika katika kulipua milipuko hiyo
Katika hali ya matukio haya ambayo yametokea kwa mfululizo, Ubalozi wa Uingereza umetoa maelezo kua wako tayari kutoa msaada wowote utakaohitajiwa katika kubaini wahusika na chanzo cha milipuko hiyo.
Mwaka jana washambuliaji wasiojulikana walishambulia makanisa mbali mbali ya kikristo na kumwagia tindikali viongozi wa Kikristo pamoja na watalii wawili waliotembelea kisiwani hapo Zanzibar.