Kasisi Francis Paul Cullen, (85) wa Kanisa Katoliki amekiri kosa la kulawiti watoto wengi pamoja na kuwatendea unyama watoto wengine wasichana baada ya kufukuzwa kutoka katika kisiwa cha Tenerife nchini Uhispania.
Katika kesi iliyokuwa ikisikilizwa jana katika mahakama mjini London, kasisi Cullen alikiri makosa 21 ya kuwatendea uchafu watoto saba.
Vitendo vya kulawiti watoto wavulana na kuwatendea unyama wasichana, vilitokea kati ya mwaka 1957 na 1991.
Msemaji wa dayosisi ya Nottingham mjini Uingereza, Kasisi Andrew Cole, amesema kuwa amefurahi kasisi huyo kukiri makosa yake.
Kasisi Cole alisema hakuna kinachoweza kuondoa masahibu yaliyowatokea watoto hao, lakini anatumaini kuwa hilo litawasaidia kwa njia moja au nyingine.
Kwa mujibu wa BBC, Kasisi Cullen atahukumiwa Machi 24, mwaka huu.
Alifanya kazi kama kasisi katika dayosisi Mackworth Parish ya Christ the King katika mtaa wa Derbyshire kati ya mwaka 1960 na 1978.
Alihamia katika kanisa ya Buxton kuanzia mwaka 1978-87 na kanisa lingine la Hyson Green, kati ya mwaka 1988-91.
Alistaafu Septemba mwaka 1991.