Muu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, Bw. Peter Toima amelazimika kukatiza ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani humo baada ya kusikia taarifa zinazodai kuwa kuna dini mpya iitwayo “Matengenezo” ambayo waumini wake hawaruhusiwi kupeleka watoto wao sekondari.
Dini hiyo pia haitaki waumini wake wawapeleke watoto wao hospitali kwa madai kuwa, Biblia ndiyo mkombozi wao.
Taarifa za kuwepo kwa dini hiyo katika Kijiji cha Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilayani humo, zilimfikia Bw. Toima juzi wakati akifanya ziara ya kukagua maendeleo ya elimu kwenye shule za sekondari katika wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo, Bw. Toima alibaini kuwa, wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza bado hawajaripoti shuleni na baada ya kuhoji, aliambiwa baaadhi yao wanakatazwa na imani zao.
Kutokana na majibu hayo, alilazimika kukatisha ziara yake na kuanza msako wa kuwasaka wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni pamoja na waumini wa dini hiyo inayowakosesha watoto haki yao ya msingi na kukiuka sheria za nchi.
Bw. Toima aliongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na watendaji wa halmashauri wakiwemo Maofisa Elimu ya Msingi na Sekondari hadi nyumbani kwa Mchungaji wa Kanisa hilo, Medard Laurent (40).
Katika nyumba hiyo, Bw. Toima na kamati hiyo iliwakuta wasichana watatu waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hawajaripoti shuleni ambapo Mchungaji Laurent alidai kuwa, sekondari wanafundisha uongo kinyume na maandiko matakatifu yanavyosema.
“Biblia imeandika kuwa, mtu aliumbwa na Mungu lakini shule za sekondari wanafundisha uongo kuwa binadamu alitokana na nyani, pia wanafundisha dunia imemeguka kutoka katika sayari wakati maandiko yanasema Mungu aliumba dunia.
“Dunia haizunguki ila jua ndilo linazunguka na siku huanza jioni saa kumi na mbili, si saa sita usiku kama walimu wanavyofundisha,” alisema Mchungaji Laurent.
Kutokana na majibu hayo, Bw. Toima aliamuru Mchungaji huyo na mabinti zake washikiliwe na Jeshi la Polisi wilayani humo wakati taratibu za kuwapeleka wasichana hao shuleni zikiendelea na Mchungaji kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Hatukubaliani na imani hii ambayo inaivuruga jamii, hatuwezi kuwaacha watoto wadogo kama hawa wapotelee kwenye imani za ajabu ajabu, nitawapeleka shule leo hii,” alisema.
Alimuagiza diwani wa eneo hilo na Ofisa Elimu Wilaya, washirikiane kuhakikisha watoto hao wanapelekwa shule na kushiriki vipindi vyote vya masomo darasani.
Kesho yake, Bw. Toima na kamati ya Ulinzi na Usalama, walikubaliana kuwa, wasichana hao Naomi Medard (16) na Anastazia Medard (14), wapelekwe sekondari zenye mabweni na kuwatenganisha ili wasiendelee kupeana ushauri wa kukataa shule.
Baada ya kikao hicho, Naomi alipelekwa Sekondari ya Nyamtukuza na Anastazia Sekondari Kanyonza ambapo binti mwingine, Beatrice Medard (19), yeye hakubahatika kuchaguliwa lakini alidai kuwa, hata angechaguliwa asingeweza kuendelea na masomo.
“Wanafunzi wanafundishwa uongo, siku nikifa sitakuwa na jibu la kwenda kumwambia Mungu kutokana na upotoshaji mkubwa wa elimu ya dunia,” alisema Beatrice.
Mchungaji huyo amezaa watoto saba kati yao wawili walifariki dunia kwa sababu ya kutopelekwa hospitali ambapo mama wa watoto hao, Bi. Julitha Sebastian (39) alipohojiwa baada ya mtoto wake mchanga kuonekana mdhoofu, alisema dini yao haiwaruhusu kwenda hospitali.
“Sijawahi kumpatia mtoto huyu chanjo ya aina yoyote wala sijawahi kujifungulia hospitali, waliokufa Biblia inasema; “Ni heri wafao katika Bwana”, alisisitiza Bi. Sebastian.
Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Elimu ya Msingi wilayani humo, Bw. Jackson Jeremiah, alisema lazima wanafunzi hao waenda shule ili waweze kutumia elimu watakayoipata kufanya utafiti ili kubaini kama ni uongo badala ya kushikilia imani ya ajabu.
“Watu wanabadilika kutokana na maisha wanayoishi na kazi wanazofanya, hakuna dini inayokataza watu wake kupata elimu, sasa nashangaa hii dini ya ‘Matengenezo’ ya aina gani hadi ikataze waumini wake wasisome au kwenda hospitali.
Naye Ofisa Elimu Sekondari wilayani humo, Florida Gandye, alisema waumini wa kanisa hilo awali walikuwa Wasabato, lakini baadaye wakajiengua na kuanzisha dini hiyo ya ajabu.
Alisema Biblia inasisitiza utii hivyo ni vyema waumini hao wakatii mamlaka iliyopo kwani imewekwa na Mungu kwa kuwapeleka watoto wao shule kama sheria inavyotaka.
Aliongeza kuwa, Serikali haipo tayari kuwaona watoto wakikosa haki hiyo kwa sababu zisizo na tija badala yake watoto hao watapelekwa shule kwa lazima na wazazi wao watachukuliwa hatua kwa kosa la kutowapeleka shule.
Katika wilaya hiyo kuna wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza, lakini hawajaripoti shule. Changamoto nyingine ni utoro na uzururaji.
Waumini wa dini hiyo wapatao saba, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa kueneza imani inayopotosha na uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
Source:majira