Maelfu ya watu wamekuwa wakihudhuria mkesha huo wa Ijumaa ya kila mwisho wa mwezi,mkesha unaoandaliwa na kituo cha Praise power Radio wakishirikiana na kanisa la Mlima wa moto.
mkesha uliojaa matendo makuu ya Mungu, shuhuda zinazogusa mioyo ya watu pamoja na kipindi cha sifa ambapo kwaya, vikundi mbalimbali pamoja na waimbaji binafsi huongoza sifa.
Pia kikundi kipya cha sifa kinachoongozwa na mwalimu John Shabani, kimekuwa gumzo katika mikesha hiyo. Kikundi hicho kinachoendelea kujifua kila wiki ndani ya kanisa la mlima wa moto, kimeendelea kupongezwa kwa kufanya vizuri.
mamia ya watu wakiongozwa sala ya toba |
Watangazaji wa Praise Power Radio - Hudson Kamoga sambamba na Veronica Frank |
Boniface Magupa, George Mpella na watu mbalimbali wakiwa makini kabisa |