Lugha hii ya Kiaramaiki inasemekana ni lugha ambayo ilikua ikitumika nchini Israel tangu mwaka 539 (KK) kabla ya Kristo hadi mwaka 7O (BK) baada ya Kristo ambapo baadae maneno yake mengi yalitafsiriwa kwa lugha ya Kiebrania na Kiarabu na kisha kutafsiriwa kwenda lugha nyingi zaidi Duniani.
Miongoni mwa wanasayansi hao kutoka nchini Uingereza ambao wapo katika mchakato huo ni pamoja na Profesa Geoffrey Khan,kutoka katika chuo kikuu cha Cambridge ambaye ameanza kwa kufanyia utafiti lahaja za lugha hiyo inayosemekana ilikuwa ikizungumzwa tangu miaka 3000 iliyopita hapa duniani,
Profesa Geoffrey Khan,kutoka katika chuo kikuu cha Cambridge |
Lugha ya Kiaramaiki ni moja ya lugha zilizopo kwenye familia ya lugha za kisemitiki na inaonekana kutumiwa zaidi sana katika vitabu vya Biblia hususan katika vitabu halisi vya Daniel na Ezra
Picha zingine za kihistoria hizi hapa chini
hili ni moja ya Sinagogi la Capernaum lililokua likitumika miaka 2000 iliyopita huu ni muonekano wake kwa sasa |
Bahari ya Galilaya,ambapo ni katika bahari hii wanafunzi wa Yesu walikua wakivua Samaki |
muonekano wa Boti hiyo kwa sasa, ambapo boti hii imehifadhiwa na kutumiwa kwa shughuli za utalii |
bustani ya Gethsemane muonekano wa kwa sasa ukiwa na miti iliyokuwepo tangu kipindi cha Yesu |
Mlima wa mizeituni unavyoonekana kwa sasa,katikati limejengwa kanisa kwa ajili ya kumbukumbu ya sehem hii ambapo inaaminika ndipo mahali Bwana Yesu alikua akienda kuomba mara kwa mara |
Western Wall moja ya sehem ambapo watu hukusanyika kwenye ukuta unaoaminika ni ukuta uliobaki ambao ni ukuta wa Hekalu lililokuwepo tangu wakat wa Yesu. |
katika ukuta huu watu hukusanyika na kufanya Ibada huku wengine wakipeleka mahitaji yao ambapo inaaminika kuna wakati Malaika hushuka kutoka mbinguni na na kuyachukua maombi,na mahitaji hayo |