Hatimaye afya ya Askofu mkuu wa kanisa la E.A.G.T na mhubiri wa kimataifa wa siku nyingi,baba wa kiroho wa wachungaji wengi nchini, kutoka Tanzania Askofu Moses Kulola sasa imerudi katika hali yake ya kawaida baada ya kuripotiwa kulazwa katika hospitali ya Bugando kwa matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokua yanamkabili .
kwa mujibu wa mtoto wa Askofu Kulola,ambaye nae pia ni mhubiri wa kimataifa na mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala mpya Mch.Daniel Moses Kulola amesema kwamba Askofu Kulola sasa ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Bugando alipokua anapatiwa matibabu na anaendelea vizuri kabisa.
wiki iliyopita chombo hiki cha habari kiliripoti juu ya kuomba maombi juu mzee wetu mpendwa Askofu mkuu Moses Kulola kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokua yanamkabili na kupelekea kulazwa katika hospitali ya Bugando kwa ajili ya uangalizi wa karibu na matibabu,
baada ya maombi ya watu wote kutoka nchi mbalimbali ambao waliipata hiyo taarifa baada ya kutembelea blog hii,blog hii imefatilia kwa karibu maendelea ya mzee wetu Moses Kulola na hadi tunakwenda mitamboni mzee Kulola anaendelea vizuri na bado ana kiu kubwa ya kuendelea kuhubiri habari za Yesu Kristo na kuwafikia watu wote duniani ili wapate wokovu, na kumjua Mungu.
kama chombo cha habari pia tunatoa shukurani kwa wote waliomuombea mzee Kulola na pia kinatoa wito tuzidi kumuombea mzee wetu ili Mungu amtie nguvu zaidi katika kuifanya kazi yake.
kwa mujibu wa mtoto wa Askofu Kulola,ambaye nae pia ni mhubiri wa kimataifa na mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala mpya Mch.Daniel Moses Kulola amesema kwamba Askofu Kulola sasa ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Bugando alipokua anapatiwa matibabu na anaendelea vizuri kabisa.
wiki iliyopita chombo hiki cha habari kiliripoti juu ya kuomba maombi juu mzee wetu mpendwa Askofu mkuu Moses Kulola kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokua yanamkabili na kupelekea kulazwa katika hospitali ya Bugando kwa ajili ya uangalizi wa karibu na matibabu,
Askofu Kulola alipokua amelazwa katika Hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza |