Jumapili hii ya tarehe 28April 2013 imekua ya aina
yake,ambapo kama kawaida Kanisa la Dar es salaam Pentecoste Church DPC
katika utaratibu wake wa kufanya Ibada kubwa ya kusifu na kuabudu kila
jumapili ya mwisho katika mwezi , Ibada hiyo katika siku hii
imefanyika kwa namna ya kipekee na yenye mvuto wa aina yake ambapo Idadi
kubwa ya wakazi wa jiji la Dar es salaam walikusanyika na kuabudu kwa
pamoja ndani ya kanisa hilo lililopo Kinondoni jijini Dar es Salaam huku Ibada hiyo ikiongozwa na kikundi cha Praise and Worship cha
Rivers of Life kutoka ndani ya kanisa hilo la DPC
John Lisu,Mwanamuziki wa nyimbo za kusifu na kuabudu nchini Tanzania alikua ni moja ya wanamuziki waliofanya vizuri katika kuongoza Ibada hiyo ya kusifu na kuabudu huku tukio hilo likipambwa pia na wanamuziki ,Bomby Johnson pamoja na timu nzima ya wanamuziki Samuel Yona,Daniel Silandah, Bale, Moses mwanamuziki mahiri katika upigaji wa Saxaphone nchini Tanzania pamoja na Aman Kapama, mwanamuziki mahiri katika upigaji wa Drums Tanzania
Tukio zima ni kama linavyoonekana katika Picha zifuatazo

John Lisu , Moses akipuliza Saxaphone |
God is able ndio jina la wimbo uliokua ukipigwa hapa wimbo ulioimbwa na Dietrick Haddon na kurudiwa tena na Darwin Hobbs wa marekani |
Palikua hapatoshi |
Bomby na Crew nzima wakiperfom wimbo wake unaoimbwa Naogelea ndani ya mto wa Damu ya Yesu |
Bomby |