Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kupokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar.
katika taarifa yake iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu taarifa hiyo imebainisha kwamba Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.
Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo.
”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushi na kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”
Aidha Rais Kikwete ameongeza kuwa “Nimeliagiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
“nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”
Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu.
WAKATI HUOHUO
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania, Muashamu Kadinali Polycarp Pengo ameelezea tukio hilo kwa masikitiko makubwa huku akiishangaa serikali na vyombo vya dola kwa kushindwa kubaini mbinu hizo chafu za mauaji ambazo dalili zake zilianza kuonekana tangu mapema...
Akifafanua suala hilo Kadinali Pengo amesema kwamba kabla ya tukio hilo kuna vipeperushi vilikua vikisambazwa kwa waislam vikiwa na ujumbe ulioandikwa na kundi la Uamsho la Zanzibar huku vikielezea kufanya matukio makubwa yatakayotikisa waumini wa dini ya kikristo Tanzania.
sehem ya kipeperushi ambacho Kadinali Pengo alikionesha kwa waandishi wa Habari ni hiki hapa.
Aidha Kadinali Pengo amewataka wakristo kutolipiza kisasi kwa yote yaliyotokea
katika taarifa yake iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu taarifa hiyo imebainisha kwamba Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.
Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo.
”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushi na kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”
Aidha Rais Kikwete ameongeza kuwa “Nimeliagiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
“nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”
Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu.
WAKATI HUOHUO
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania, Muashamu Kadinali Polycarp Pengo ameelezea tukio hilo kwa masikitiko makubwa huku akiishangaa serikali na vyombo vya dola kwa kushindwa kubaini mbinu hizo chafu za mauaji ambazo dalili zake zilianza kuonekana tangu mapema...
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania, Muashamu Kadinali Polycarp Pengo |