Siku moja baada ya Padri Evarist Mushi wa kanisa Katoliki Zanzibar kuuwawa kwa kupigwa Risasi wakat akiwa anaelekea kanisani kuendesha Misa siku ya jumapili, jumanne hii 19February 2013 watu wasiojulikana wamevamia moja ya kanisa lijulikanalo kama Shalom lililopo kusini Unguja na kufanya jaribio la kuliteketeza kwa moto.
kwa mujibu wa post zilizowekwa asubuhi mapema katika mtandao wa Jamii forum habari zilikua zinasema kwamba
"Taarifa za kuaminika zilizorushwa na Radio Wapo Fm ya jijini Dar es Salaam katika kipindi chake cha patapata leo asubuhi, ni kwamba watu wasiojulikana wamelivamia kanisa moja huko Zanzibar na kulirushia kitu kama bomu kilicholipuka moto japo majirani waliamka na kuuzima moto huo kabla kuleta madhara makubwa.
Tukio hilo limejitokeza asubuhi ya leo kwenye mida ya saa kumi.
kujiridhisha zaidi nimechek na post ya ITV facebook nao wamepost
ITV Tanzania
Muendelezo wa Habari ya kuchomwa kanisa ZANZIBAR:Kamishna wa Polisi Kusini Unguja,
AUGUSTINO OLOMI amethibitisha kuwa kanisa lilichomwa moto ni Kanisa la SHALOM.