HOFU ya kuwapo kwa magaidi wa mtandao wa
Al- Qaeda, imetanda katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza baada ya
kuvuja kwa taarifa za kuanzishwa kwa chuo kimoja cha kidini
kinachohofiwa kutoa mafunzo yenye mwelekeo wa kigaidi visiwani humo.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa chuo
hicho kinajulikana kwa jina la Markaz, Aljazeera na kimeanzishwa kwa
ufadhili wa raia wa kigeni ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu.
Makundi yanayotajwa kufadhili uendeshaji
wa chuo hicho ni AI-Qaeda na AI shabab yanayoaminika kuwa na mtandao
mkubwa wa ugaidi duniani. Uchunguzi uliofanywa na Mtanzania Jumatano
wilayani Ukerewe, umebaini kuwa chuo cha Markaz kinatoa rriafunzo kwa
watu wa rika mbalimbali yenye mwelekeo wa kujihami na kushambulia kama
Karate na Kung-fu.
Kikundi cha Alshabaa mafunzoni |
Aidha, taarifa nyingine za kiuchunguzi
ambazo gazeti hili lilidokezwa na wakazi wa kisiwani humo walioonyesha
wasiwasi wa kuwepo kwa chuo hicho, zilidai’ kuwa, aina nyingine ya
mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho na kushambuliana kwa silaha aina
ya jambia. Uchunguzi ulibaini zaidi kuwa, wanafunzi katika chuo hicho ni
watoto wenye umri wa kati ya miaka sabahadi 10 na pia kuna wanafunzi
vijana na watu wazima.
Baadhi ya wakazi wa wilayani humo waliopata
kufanya kazi katika chuo hicho, waliliambia gazeti hili kuwa chuo hicho
kimekuwa kikipokea mizigo ya aina mbalimbali, ikiwa imefungwa kwenye
maboksi ambayo katika udadisi wao walibaini kuwa, baadhi ya bidhaa
zinazokuwa kwenye shehena hizo ni kanzu, seti za televisheni, vitabu na
silaha za aina mbalimbali.
mfano wa mafunzo ya kivita ambayo hutolewa na kikundi cha alshabaab kwa kundi la watoto |
Walidai kuwa, walianza kukitilia mashaka
chuo hicho baada ya kubaini kinapokea silaha katika baadhi ya mizigo
yake. Mbali ya hilo, wakazi hao walilieleza gazeti hili kwamba aina ya
wageni ‘ wanaoingia na kutoka visiwani humo kwa minajili ya kukitembelea
chuo hicho, ni jambo jingine ambalo limekuwa ‘likiwafanya wazidi
kukitilia shaka chuo hicho.
mfano wa mafunzo ya kivita ambayo hutolewa na kikundi cha alshabaab kwa kundi la watoto |
Kwa mujibu wa wakazi hao, wageni hao
wamekuwa wakiingia kisiwani kwa njia ya mitumbwi wakipita katika njia za
panya nyakati za usiku.
Wageni hao kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo la
Nansio ni wale wanaodaiwa na kuaminika kutoka katika nchi jirani za
Kenya na Uganda ambazo mipaka ya Ziwa Victoria inapita.
Wa f a n y a b i a s h a r a
wanaojihusisha na usafirishaji abiria waliozungumza na gazeti la
Mtanzania Jumatano walieleza kuwa, wageni wanaowapakia kuwapeleka chuo
cha Markaz au maeneo mengine ya kisiwa hicho huwalazimisha kuondoa
misalaba waliyoivaa shingoni au waliyotundika katika magari na pia
huwataka wazime redio katika magari yao.
Hofu hiyo ya wakazi wa Nansio
ilisababisha gazeti hili kumtafuta Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli
(Chadema) ambaye naye alikiri kulifahamu jambo hilo. Akizungumza
kupitia simu yake ya kiganjani, Machemli alisema chuo hicho kinatoa
mafunzo ambayo wakazi wake wanayahusisha na matendo ya kigaidi.
Mbunge huyo alisema hofu zaidi kuhusu
chuo hicho ni kuwapo kwa taarifa zinazodai kwamba, baadhi ya wanachuo
ambao wamewahi kupata mafunzo chuoni wanatajwa kuwa wanachama wa makundi
ya kigaidi ya AI Qaeda na AI-Shabab.
Kwa mujibu wa mbunge huyo,
miongoni mwa hatua ambazo amepata kuzichukua ili kutafuta majibu ya
wasiwasi wa wananchi wa Ukerewe ni pamoja na kumsaka mmoja wa watu
anayekijua chuo hicho.
“Ni kweli tuna wasiwasi na hatuoni kazi ya umma
kinachojihusisha nacho. Niliwahi kumuuliza Diwani wa Kata ya Nansio,
Sheikh Ramadhani Mazige (CCM) kuhusu uhalali wa kuwapo kwa chuo hicho
kwa sababu alikuwa akisimamia ujenzi wake na nikashauri juu ya umuhimu
wa kubadili aina ya mafunzo yanayofundishwa chuoni hapo na jibu lake
lilikuwa wenye chuo hawataki.
Alipoulizwa iwapo anawafahamu
wamiliki wa chuo hicho, alikana kuwatambua kwa kueleza kuwa, jitihada
zake za kuwafahamu hazikufanikiwa baada ya Diwani Mazege kukataa
kuwataja.
Machemli alisema kuwa, amepanga kulifikisha suala hilo kama
hoja binafsi kwenye Baraza la Madiwani ili kuomba kibali cha kutembelea
chuo hicho kuona shughuli zinazofanyika na kwamba iwapo atakwamishwa,
atalifikisha suala hila katika ngazi za juu.
Akizungumza kuhusu raia wa kigeni
wanaopitia njia za panya kwa usafiri wa mitumbwi nyakati za usiku kufika
chuoni hapo, Machemli alisema hilo hawezi kulipinga.
Kwa mujibu wa
Machemli, jiografia ya visiwa vya Ukerewe inavifanya viwe wazi kuhusu
mipaka yake na kwamba jambo hila alipata kulizungumza bungeni ingawa
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha
alimpuuza.
“Nilizungumza katika mkutano uliopita wa Bunge kuhusu mipaka
ya Ukerewe kuwa wazi sana, nililalamika kwamba, wanajeshi wa Kenya na
Uganda wanakuja hadi katika kisiwa hicho kufanya mazoezi yake na
kuondoka, lakini nashangaa waziri akanipuuza,” alilalamika Machemli.
Alipotafutwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mwanza,Ernest .Mangu kwa ajili ya kuzungumzia juu ya hofu hiyo, alisema
anaomba apewe muda kwa sababu yeye ni mgeni mkoani humo na huu mwezi wa
pili akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, hivyo yapo mengi ambayo
hayafahamu.
Hata hivyo, Mangu aliliahidi gazeti hili kufuatiliajuu ya
suala hila na kulitolea ufafanuzi baadaye. Kwa up an de wake, Mkuu wa
Wilaya ya Ukerewe, Mary Tesha alikana kufahamu chochote na badala yake
akahoji sababu za mwandishi kumtafuta wakati tayari suala hila
lilisharipotiwa katika gazeti hili hivi karibuni.
Kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa vikundi
vinavyojihusisha na utoaji mafunzo ya . kigaidi hapa nchini, vikiwa
vimejificha katika mwamvuli huku lengo halisi likiwa kuhatarisha amani
ya kitaifa.
Tayari Rais Jakaya Kikwete amekwishaagiza kusakwa kwa
makundi yenye mwelekeo huo yanayohisiwa kuhusika na machufuko na mauaji
hapa nchini, wakati akitoa salamu za pole baada ya tukio la kuuawa
kinyama kwa Padre wa Kanisa Katoliki Evaritus Mushi huko visiwani
Zanzibar.
Mwisho.
Kwa habari zaidi fuatilia mfululizo wa makala kuhusu hofu
hiyo ya ugaidi kisiwani Ukerewe katika ukurasa wa 15 wa gazeti hili.–Mtanzania
20/Februari/2013