Kufuatia mvutano mkali baina ya Wakristo na Waislam ulioibuka kata ya Nyehunge,wilayani Sengerema jijini Mwanza ukihusisha suala la kuchinja wanyama mbali mbali kwa ajili ya kitoweo ,mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo atoa tamko la serikali kwa mkoa wa Mwanza linalobainisha nani ana haki ya kuchinja wanyama.
Mhandisi Evarist Ndikilo mkuu wa mkoa wa Mwanza |
hali hiyo imekuja baada ya wakazi wa kata hiyo ya
Nyehunge kuwa na mgogoro ulioanza tangu mwezi june mwaka jana ukihusisha
wakristo kutaka kupewa mamlaka ya kuchinja wanyama kama ilivyozoeleka
kwa waislam kwenye machinjio.
kufuatia mgogoro huo, mkuu wa mkoa wa Mwanza alifanya
ziara katika kata hiyo siku ya alhamisi,January 10, 2013 ambapo miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja
na suala hilo la kuchinja wanyama.
Mhandisi Evarist Ndikilo mkuu wa mkoa wa Mwanza |
"Natoa msimamo wa serikali ya mkoa wa Mwanza kuhusu mgogoro huu ambao ndani yake kuna udini,Hatuwezi kuchezea amani ya kijiji cha Nyehunge na taifa letu .kuanzia leo tutachinja kwa utaratibu wetu wa siku zote wa waislam kuchinja Nyama."
kwa mujibu wa gazeti la la Sauti ya Afrika la jijini Mwanza toleo number 004 la January 13-19, 2013.. Limeeleza kua baada ya msimamo huo wa serikali kauli hiyo iliibua sintofaham baada ya baadhi ya wananchi kuanza kusambaa huku wakidai
"Hatuoni kilichokuleta,hebu tuondoke,Hatutaki"
huku mkuu wa mkoa akiwajibu " Jaribuni muone,,,ndio maana nimekuja hapa na kamanda wa polisi wa mkoa"""
kupitia mkutano huo pia mkuu wa mkoa alipiga marufuku kuwepo kwa bucha za waislam na wakristo ambazo zilikua tayari zimeshaanza kushamiri na kusababisha baadhi kukosa wateja kutokana na itikadi za kidini.
wakati huo huo Kiongozi wa kanisa la Tanzania Field Evangelism Bishop Augustine Mpemba amekua mstari wa mbele kupitia kituo cha radio maarufu kama Radio Kwa Neema FM ya jijini Mwanza ambapo
Bishop Augustine Mpemba Kiongozi wa kanisa la Tanzania Field Evangelism |
Katika kipindi cha mwaka jana ajenda ilikua ni kuhamasisha wakristo kua na haki ya kuchinja wanyama kwa ajili ya kitoweo na si kutoa jukumu hilo kwa waumini wa dini ya kiislam.
Bishop Augustine Mpemba akisalimiana na Mh.Rais Jakaya Kikwete,nyuma kidogo mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo |