Rais Barack Obama wa Marekani anatarajia kula kiapo cha kuliongoza taifa hilo la Marekani katika kipindi kingine cha pili cha miaka minne mnamo January 21 Mwaka huu 2013,kiapo kitachoambatana na utumiaji wa Biblia kitabu kinachotumiwa katika dini ya kikristo duniani kote.
Rais Obama akila kiapo kuliongoza taifa la Marekani katika kipindi cha miaka minne ya kwanza |
katika kula kiapo hicho Rais Obama anatarajiwa kushikilia Biblia mbili, tofauti na awali ambapo katika kiapo chake cha kuliongoza taifa la Marekani katika miaka minne ya mwanzo,alitumia biblia moja katika kula kiapo.
wakati huu Rais Obama anatarajiwa kutumia Biblia zilizokuwa zikimilikiwa na Abraham Lincoln na nyingine iliyokua ikimilikiwa na Martin Luther King Jr.
Abraham Lincoln |
Martin Luther King Jr. |
Kwa taifa la Marekani,kutumika kwa biblia ya kifalme wakati huu kunachukuliwa kama tendo muhimu kwa sababu siku ya kiapo hicho imeangukia siku ya tarehe 21 January siku ambayo taifa hilo linaadhimisha siku ya mashujaa kwa kukumbuka na kuwaheshimu Viongozi,Mashujaa waliouwawa wakati wa kupigania haki za kiraia chini Marekani miaka ya nyuma.
Miongoni mwa viongozi wanaokumbukwa katika siku hii ya mashujaa nchini Marekani ni pamoja Martin Luther King jr aliyewahi kutoa speech iliyobeba ujumbe " I have a dream" miaka 50 iliyopita
Martin Luther King Jr. |
katika kiapo chake cha kwanza cha kuliongoza taifa hilo kwa miaka minne iliyopita ,Rais Obama alitumia Biblia ya Lincoln.
George Washington rais wa kwanza wa Marekani |
ijapokuwa marais wengi waliopita wamekuwa wakitumia biblia moja katika kula kiapo cha urais, Rais Obama anakuwa sio wa kwanza kutumia biblia mbili katika kiapo cha urais kwani marais wengine waliowahi kutumia Biblia mbili ni pamoja na Harry Truman alifanya hivyo pia mnamo mwaka 1949, pia Dwight Eisenhower aliyefanya hivyo mwaka 1953 na Richard Nixon pia alifanya hivyo mnamo mwaka 1969
Rais George W. Bush pia aliwahi kutumia biblia katika kiapo chake ambapo katika kula kiapo alitumia kitabu cha Isaya 40:31 chenye ujumbe "bali wao wamngojeao Bwana,watapata nguvu mpya watapanda juu kwa mbawa kama tai,watapiga mbio wala hawatachoka,watakwenda kwa miguu wala hawatazimia.