
kikawaida wanamuziki wengi wa Tanzania hususan wanapokuwa wametembelea sehem flani au nchi flani kwa huduma,aina ya mapokezi ambayo imezoeleka ni kwa mwanamuziki kupokelewa na mashabiki au wenyeji wake kumpokea kwa shangwe na kelele wakat mwingine mapokezi yaweza kuwa ni crew ya watumishi katika eneno hilo huku wakiwa wamevalia smart na baadhi ya zawadi mikononi kama ishara ya kumfanya mgeni ajisikie furaha katika kuingia eneo hilo
Kwa flora mbasha na mumewe ,Emanuel Mbasha hali ilikua tofauti baada ya kukuta wenyeji wake wakimpokea kwa mitutu ya Bunduki lakini kwa Amani kabisa ikiwa ni ishara ya kumhakikishia ulinzi wa kutosha akiwa nchini Congo kama inavyoonekana katika picha alizozipost Flora mbasha katika wall yake ya Face book
![]() |
Emannuel Mbasha Mume wa Flora Mbasha akiwa katika escort nzito toka kwa wanajeshi nchini Kongo |
Flora mbasha ni moja ya wanamuziki wakubwa nchini Tanzania ambaye huduma yake ilianzia jijini Mwanza katika kanisa la Bugando EAGT aiwa kama mwanakwaya na baadae Mungu amemunua na kufika ngazi ya juu kabisa hadi kupata mialiko ya kimataifa ikiwa ni katika nchi kama Marekani,na nchi nchi nyingi za Afrika mashariki na kati
![]() |
Flora Mbasha na mumewe, Emannuel Mbasha wakiwa na Rais Jakaya Kikwete Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
![]() |
moja ya perfomance ambazo flora mbasha na crew yake walizifanya wakiwa Marekani |
moja ya video ambayo flora Mbasha aliifanya alipokuwa Marekani ni hii hapa
wimbo unaitwa I give my life to you by Zack Ponio akimshirikisha Flora Mbasha na NYC man ikiwa ni dedication kwa watoto wa Mungu duniani kote
![]() |
Waziri mkuu wa Kenya Laira Odinga na Mhe Magufuli waliposhindwa kujizuia na kupanda jukwaani kucheza wakati Flora Mbasha akiimba |
![]() |
Emanuel Mbasha katika moja ya huduma ambazo wamekuwa wakifanya katika kumtukuza Mungu |
Na injili isonge mbele
ReplyDelete