kongamano hilo limeanza leo asubuhi siku ya jumanne 24July 2012 katika ukumbi wa Shinyanga Hotel jijini mwanza,na limewahusisha wachungaji toka wilaya zote za jiji la mwanza ikiwa ni pamoja na Magu,Nyamagana,Ilemela,Sengerema,na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa ikiwa ni pamoja na mkoa mpya wa Geita,kwa lengo la kuwaweka wachungaji pamoja na kupeana mbinu za kuujenga mwili wa kristo.
akiongea na blog hii Muinjilist Peter Pretorious ameeleza kuwa Jesus alive Gospel Outreach sio club, chama,dhehebu,wala kanisa bali ni huduma yenye kuwaunganisha wachungaji toka makanisa mbali mbali ya kipentekoste kwa lengo la kuihubiri injili ya Yesu Kristo Duniani kote bila mipaka hivyo Lengo kuu la kongamano hilo ni kuwapa mbinu mbali mbali wachungaji ili waweze kufika kila kona ya nchi na kuhubiri ili watu wengi wamjue Yesu Kristo kisha waishi maisha yanayompendeza Mungu.
na baadae kikundi cha kusifu na kuabudu kilipata fursa ya kuhudumu kwa nyimbo za kusifu na kuabudu
huku wachungaji wakiingia katika uwepo mzito wa Roho mtakatifu katika maombi na ndipo Muinjilist Peter pretorious alipoanza kuhubiri huku akiandamana na mkalimani wake mchungaji Eugene Mulisa toka High way of Holines cathedral la jijini Mwanza.
Peter pretorious ni moja ya wahubiri wa siku nyingi ambao walikuwa wakija nchini Tanzania miaka ya 1990 na kuhubiri katika mikutano mikubwa sana iliyokuwa ikikusanya maelfu ya watu waliokuwa wakihudhuria na kumpa Yesu maisha yao baada ya kuguswa na neno la Mungu lilikoa likihubirwa katika mikutano hiyo.
kushoto ni pastor Eugene Murisa akiwa na Ev.Peter Pretorious |