Pastor Darwin Hobbs |
sauti yake yenye nguvu ya ajabu imekuwa ni moja ya vitu vinavyoupamba mziki wake na kumfanya aendelee kupendwa na watu na kukubalika na watu wote waliopata kusikiliza au kutazama nyimbo zake sehem mbali mbali Duniani.
Historia yake ya Kimuziki inaonyesha kuwa Darwin Hobbs alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 10,huko Nchini Marekani.wakati huo Darwin Hobbs alianza kuonyesha uwezo wa kuimba katika kanisa ambalo Mama yake mzazi alikua anasali...
Tofaut na wanamuziki wengine ambao uwezo wao wa kuimba umekuja baada ya kupata mafunzo katika kwaya au vikundi vya muziki walivyopo lakini Darwin Hobbs anasema kuwa Mungu alimbariki kwa karama ya uimbaji tangu akiwa na umri wa miaka 10 bila kuwa na mafunzo yoyote ya mziki au uimbaji
katika miaka ya 1990 Darwin Hobbs anasema milango ilianza kufunguka zaidi kwani alianza kupata mialiko mingi zaidi baada ya ya kuhamia Nashville na kujikita zaidi katika career ya Music ambapo alianza kupata mialiko zaidi ya 700 kuimba katika stage kubwa kama ilivyo kwa wanamuziki wengine kama Michael W. Smith, Twila Paris, Michael Card, CeCe Winans, Donnie McClurkin.
katika yote hayo Darwin Hobbs maisha yake yalikua yamegubikwa na uchungu,na Huzuni kwani ni mmoja wa watoto waliolelewa na Mama yake na Baba wa kambo baada ya mama yake kupewa talaka na baba yake,
Mama yake Darwin Hobbs aliamua kuolewa na mtu mwingine baada ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika na baba wa kambo wa Darwin ndiye aliyemtia Moyo Darwin kwa kumuendeleza kuhuduma katika kanisa lake ambapo Darwin alikua akipewa nafasi za kuimba kanisani.
Darwin anasema marakwa mara amekua akitumia huduma hii ya kuimba kama njia pia ya kumfariji mama yake kwa shida,na maumivu moyoni yaliyotokana na maisha waliyokua wakiishi baada ya baba yao kumwacha mama yake.
Darwin amezidi kumpa heshima yake baba yake huyu wa kambo kama mtu muhimu katika familia yao aliyemuendeleza kihuduma baada ya kupitia shida na tabu nyingi akiwa mtoto mdogo lakini hadi sasa Mungu amemuinua na kumfanya kuwa mmoja wa wanamuziki wakubwa Duniani wanaoimba mziki wa injili.
Hadi sasa Darwin Hobbs ameshatoa albums ambazo ni pamoja na
- Mercy (EMI Gospel, 1999)
- Vertical (EMI Gospel, 2000) (Billboard Gospel #26)
- Broken (EMI Gospel, 2003) (Billboard Gospel #3)
- Worshipper (EMI Gospel, 2005) (Billboard Gospel #8)
- Free (Tyscot Records, 2008)
- Champion (Imago Dei Music Group, 2010) (Billboard Gospel #6 pia Darwin Hobbs ameshawahi kutoa single ambazo pia zilipata mafanikio katika soko la Muziki na kihuduma pia ,moja ya single hizo ni pamoja na
- "Everyday"
- "Nobody Like Jesus"
- "Beautiful To Me"
- "Free"
- "Champion"
Picha zaidi za pastor Darwin Hobbs zipo hapa chini
Pastor Darwin Hobbs na mkewe Traci Hobbs |
Pastor Darwin Hobbs akiwa na wadau wa Muziki wa injili nchini Marekani katika uzinduzi wa moja ya album ya Darwin Hobbs |
Pastor Darwin Hobbs na mkewe Traci Hobbs |