Wakifundisha kwa nyakati tofauti Watumishi hao wa Mungu wameelezea umuhimu wa kupata maarifa na ufahamu utakaomuwezesha mkristo kutambua haki zake za urithi toka kwa Mungu na kuwa katika nafasi nzuri ya kupokea urithi huo ambao umekwisha andaliwa na Mungu ambao huambatana na baraka za rohoni na mwilin.
Kongamano kubwa la kiroho likiwa na kauli mbiu ya Urithi wa Kiungu (Devine Heritage) limefanyika jumapili hii jijini Mwanza na kuhudhuriwa na mamia ya watu toka kada mbalimbali na kutoa mafundisho ya kiroho kwa makundi tofauti tofauti ya watu ikiwa ni pamoja na makundi ya vijana wazee na wasomi wa vyuo vikuu vya jiji la Mwanza
Kongamano hilo lililoanza mida ya saa tisa alasiri mpaka saa 12jioni awali lilitanguliwa na vikundi mbalimbali vya sifa na kuabudu ikiwa ni pamoja na Tafes Saut, CBCI Band, New Creation Band na mwimbaji binafsi Epafrodito
Wazungumzaji wakuu ambao walipata fursa ya kuzungumza katika kongamano hilo ni pamoja na Mchungaji Goodluck Kyara kutoka kanisa la NVCC la jijini Mwanza, Mchungaji Denis Sebastian Kiandika kutoka kanisa la MICC -Mwanza, na na Mchungaji Bill Brown ambao kwa pamoja waliweza kuzunguza na kuwasilisha jumbe mbalimbali za kiroho zikiwa na mafundisho ya kumjenga muamini katika kuuelewa urithi wa kimungu ndani ya Maisha ya Mwanadamu hususani katika kipindi hiki cha sasa.
Mchungaji Bill Brown |
Baadhi ya picha za kongamano hilo ni kama zinavyoonekana hapa chini