kutoka Shirika la utangazaji la BBC limeripoti kwamba Maafisa wa polisi katika wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera Tanzania wanafanya uchunguzi kufuatia kuteketezwa kwa makanisa matatu eneo hilo.
Makanisa yaliyochomwa moto ni Pentecostal Assemblies of God (PAG) eneo la Buyekera, Living Water International na Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAG) kata ya Kibeta yote ya mjini Bukoba.
Kamishna msaidizi wa polisi wilaya ya Bukoba Agastine Olomi amesema hakuna yeyote aliyeripotiwa kufariki au kujeruhiwa katika visa hivyo.
taarifa za watu kuuawa ama madhara yoyote kwa binadamu
“Tunafanya uchunguzi kubaini kiini na wahusika wa hili tukio. Ni mapema sana kutupia lawama watu fulani kwa hivyo tunawataka wananchi kusubiri uchunguzi ufanyike,” ameambia mwandishi wa BBC Esther Namuhisa.
Kati ya makanisa hayo yote, ni moja tu lililokuwa na mlinzi.
Kwa upande wao, viongozi na wahubiri katika makanisa hayo wametoa wito kwa vyombo vya dola kuharakisha uchunguzi huo ili kubaini wahusika.
Mchungaji David Mshana, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa makanisa hayo katika mkoa huo ulio kaskazini magharibi mwa Tanzania, amesema hiyo sio mara ya kwanza kwa makanisa kuripotiwa kuchomwa moto eneo hilo.
Baadhi ya viongozi wa makanisa hayo wamelaumu vyombo vya dola wakidai vimeshindwa kuyatafutia ufumbuzi mashambulio hayo ya makanisa madogo.
Wamesema hilo linaibua hofu kuhusu usalama wa makanisa makubwa.
Hii ni mara ya sita kwa makanisa kuchomwa moto katika kipindi cha mwaka mmoja eneo la Kagera |