Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Milca Kakete Milca Kakete ambaye kwa sasa anaishi nchini Canada,amefanya uzinduzi wa album zake mbili zenye nyimbo za Injili,Uzinduzi uliofanyika katika Kanisa la VCCT mbezi beach jijini Dar es Salaam,chini ya Mchungaji kiongozi Dr.Huruma Nkonne.
|
Mwanamuziki Milca Kakete |
Katika Uzinduzi huo na kuwekwa wakfu kwa Album hizo mbili za Gospel ,Mwanamuziki huyo alieleza lengo kuu la mauzo ya Album hiyo kua kiasi cha pesa ambacho kitapatikana kuanzia katika uzinduzi huo na mauzo yake kitaelekezwa kwenye kuwawezesha watumishi wa Mungu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wachungaji na wainjilist waliopo maeneo ya vijijini ili wanunuliwe usafiri kuanzia Baiskeli,na Pikipiki ili ziwasaidie katika usafiri katika kuwafikia watu wengi vijijini na kuwafikishia neno la Mungu.
uzinduzi huo ulisindikizwa na wanamuziki wengine wa nyimbo za Injili ikiwa ni pamoja na Kundi la The Voice,Miriam Mauki, Angel Magoti, na Vikundi vingine vingi vya nyimbo za injili
|
Kundi la The Voice likamtambulisha Prosper Mwakitalima kama member mpya ndani ya kundi hilo |
|
Mch Dr Huruma Nkone (kushoto) akiwa nana mkewake. |
|
Mch Safari wa kanisa la D P C jijini Dar na Milca Kakete akiteta jambo
na mmoja wa marafikizake wa karibu sana waliohudhulia ukumbini |
|
Mama yake mzazi wa Mwimbaji Milca Kakete aki mkumbatia mmoja ya
wanafamilia baada ya kutoka jukwaani alipokua akitoa neno la shukrani
kwa Mung,mama huyo alidondosha chozi la furaha kwakitendo
alicho kishuhudia,kwani ilikua ni moja ya maombi yake kwa Mungu ampatie
japo hata mmoja ya watoto wake atakae weza kuwa mrithi wake,kwani na yeye
ni mwimbaji wa miaka mingi saana. Licha ya kuwa mzee sasa lakini Bado
anamtumikia Mungu kwa Uimbaji. |
|
Mama yake mzazi wa Milca Kakete akitoa shuuda na shukrani |
|
Mwanamuziki Mwatshy moja ya watu waliofanya perfomance ya nguvu kwa nyimbo zake zenye mahadhi ya Kikongo a.k.a Sebene |