JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia wafuasi 15 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Josephat Gwajima.
Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam, baada ya kupata mshituko wakati akihojiwa na makachero wa Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, ilisema usiku wa kumkia jana, mmoja wa walinzi wa Hospitali ya TMJ alibaini njama za kutaka kutoroshwa kwa Askofu Gwajima ambapo alitoa taarifa polisi.
“Kutokana na hali hii, makachero wa polisi walifika eneo hilo na kukuta kweli kuna hali ambayo si ya kawaida kwa kuwapo kundi la watu.
“Wamekamatwa watu 15 na mmoja wao Ekomia Diagare, alikutwa na begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali ambayo alidai anampelekea Askofu Gwajima.
“Bastola aina ya Bereta yenye namba CAT 5802 ikiwa na risasi 3, risasi 17 za Shortgun, vitabu, hundi za benki, hati ya kusafiria yenye jina Gwajima Mathias Joseph yenye namba AB54480,” alisema Kamanda Kova.
Mbali na hilo, pia inadaiwa watu hao walikutwa na kitabu cha Benki ya Equity na hundi, nyaraka mbalimbali za Kampuni ya Puma, chaja za simu na suruali mbili, makoti mawili, fulana za ndani moja,soksi jozi mbili na nguo ya ndani.
Kamishna Kova, aliwataja watuhumiwa weingine kuwa ni Chitama Mwakibambo (32) , Edwini Audex (24) , Adamu Mwaselele(29), Frederick Fusi (25), Frank Minja(24), Emmanuel Ngwela (28).
Wengine ni Geofrey William (30), Mchungaji Mathew Nyangusi (62), Mchungaji Boniface Nyakyoma (30), Geofrey Andrew (31), Mchungaji David Mgongolo (24), George Msava (45), Nicholaus Patrick (60) na Mchungaji George Kiwia(37).
MTANZANIA ilimtafuta Wakili wa Askofu Gwajima, John Mallya kuhusu taarifa hizo, alikiri kukamatwa kwa watu hao kutokana na njama hizo.
MAASKOFU WAWASILI DAR
Wakati huo huo, maaskofu na waumini wa kanisa hilo kutoka mikoa mbalimbali, wamewasili jijini Dar es Salaam ili kufuatilia afya ya kiongozi wao.
Waumini hao walianza kujitokeza jana saa 2 asubuhi katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe ambako ndiyo makao makuu ya kanisa hilo.
Hali katika uwanja huo, ilikuwa tulivu huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na watu wote ambao walionekana si waumini wa kanisa hilo, wakiwamo waandishi wa habari wakibainika mapema.
Ilipofika saa 5:30 asubuhi, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Gwandu Mwangasa alianza kuwatambulisha maaskofu na wawakilishi waliotoka mikoa mbalimbali ili waweze kutambuliwa na waumini wenzao.
Mchungaji Mwangasa, aliitaja mikoa ambayo viongozi na maaskofu wamefika Dar es Salaam kuwa ni Lindi, Geita, Shinyanga, Mwanza, Morogoro na Iringa.
Mikoa mingine, ni Singida, Arusha, Tabora, Njombe, Tanga na Dodoma.
Katika ibda hiyo, baadhi ya waandishi wa habari na wapiga picha walifukuzwa na viongozi wa kanisa hilo kwa madai kuwa hawana kibali cha kuwepo mahali hapo.
ASIMULIA MKASA
Mwangasa ambaye pia ni msemaji wake, alisema wiki iliyopita, Askofu Gwajima alikuwa Arusha katika kikao cha maaskofu wa Kipentekoste ambacho kilikuwa kinajadili mambo mbalimbali.
“Wakati kikao kinaendelea, tuliona taarifa kwenye vyombo vya habari ambazo zinaeeleza anaitwa Kituo cha Polisi Kati ili akahojiwa kwa tuhuma za kumtukana, Kardinali Pengo,”alisema Mwangasa.
Mchungaji Mwangasa, alisema baada ya kupata taarifa hizo, Askofu Gwajima alisitisha shughuli zake na kurudi Dar es Salaam kuitikia wito wa polisi.
Alisema walipofika polisi, kila mmoja alihojiwa kwa nafasi yake, lakini baada ya kutoka kuhojiwa, Gwajima alionekana amelegea na kuchoka.
“Tulipoona hivyo, tukamuuliza polisi wamekufanya nini?, alitujibu hawajamfanya chochote zaidi ya kumhoji,”alisema.
“Polisi walifanya kazi yao kwa mujibu wa sheria wala hakuna tatizo lolote lililopo baina yake na polisi na kwamba alijibu kulingana na alivyoulizwa: alisema Mchungaji Mwangasa.
Alibainisha baada ya gwajima kusema hivyo, alianguka na kuzimia, kitendo ambacho kiliwafanya polisi kumkimbiza Hospitali ya polisi iliyopo Kurasini kwa ajili ya matibabu.
Alisema walipofika huko, Gwajima alizinduka na kukataa kutibiwa na madaktari wa hospitali hiyo huku akiomba kwenda kutibiwa hospitali ya TMJ ambako kuna daktari wake.
Mchungaji Mwangasa aliendelea kusema kuwa madaktari walikubaliana na Gwajima kwa sharti la kumtaka asaini maelezo ya kukataa kutibiwa kwenye hospitali hiyo na kwenda TMJ.
Kutokana na hali ilivyokuwa, madaktari wa polisi waliwaambia kuwa utaratibu wao ni lazima mgonjwa uyo aandikiwe rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kwa ajili ya matibabu.
“Tulipofika Muhimbili,Gwajima alizinduka tena na kukataa kutibiwa na madaktari wa hospitali hiyo na kudai apelekwe TMJ kwa sababu kuna daktari wake.
“Wakati wanajadiliana suala hilo alitokea daktari wake ambaye aliandika rufaa ili aweze kupelekwa hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu” alisema Mchungaji Mwangasa.
Shitaka la pili alidai liliripotiwa na mtu mmoja mwenye majina matatu ya kiislamu ambaye alifungua kesi ya madai ya kumtukana Pengo.
Alisema katika shitaka hilo, mtu huyo aliitaka serikali kumchukulia hatua Gwajima kwa kosa hilo kwa sababu alimdhalilisha kiongozi huyo wa kiroho.
“Sisi hatuna ugomvi na Waislamu, lakini kesi ile haikufunguliwa na Pengo wala mkatoliki yeyote, bali imefunguliwa na mtu ambaye majina yake yote matatu yanaonyesha niya kiislamu, sasa hatujui nini kimetokea,”alisema Mchungaji Mwangasa.
JUKWAA LA KIKRISTO
Mchungaji Mwangasa, alisema Jukwaa la Kikristo lina utaratibu wake wa kumuadhibu kiongozi wa dini anayekwenda kinyume na utaratibu.
Alisema tayari jukwaa hilo, limeandaa utaratibu wa kushughulikia suala hilo.
Alisema kulipeleka suala hilo polisi ni kinyume na utaratibu wa jukwaa hilo ambao limelenga kulidhohofisha kanisa.
GWAJIMA AIMARIKA
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jana, mke wa Askofu Gwajima,Grace Gwajima alisema afya ya mume wake imeanza kuimarika, licha ya kuendelea kulazwa chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).
Alisema kama hali ikiendelea hivyo mpaka leo, watafanya utaratibu wa kumtoa ICU na kumhamishia chumba cha kawaida.
“Askofu anaendelea vizuri,anaongea na anaweza kula leo (jana)… tunamshukuru Mungu kwa hilo,” alisema Grace.
Askofu Gwajima,alizimia mwishoni mwa wiki wakati akihojiwa katika kituo Kikuu cha Polisi mjini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutoa lugha za matusi na kashfa dhidi ya Kardinali Pengo.
Katika hatua nyingine, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo amevunja ukimya na kusema amemsamehe kutoka moyoni Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Kardinali Pengo ametoa kauli hiyo, ikiwa ni siku chache tu baada ya Askofu Gwajima kumshambulia kwa maneno makali yaliyosababisha aitwe polisi kuhojiwa.
Kardinali Pengo, alitoa kauli hiyo,wakati wa mahubiri ya misa takatifu ya matawi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu mjini Dar es Salaam jana.
“Sina kinyongo na Askofu Gwajima na kwamba nimemsameha kwa yote aliyosema.
“Ndugu zangu waamini naomba kueleza au kutamka kwa kila mmoja wenu kuhusu maneno yaliyozuka hivi karibuni.
“Kutoka ndani ya moyo wangu kwa yeyote aliyesema hayo,mimi natoa msamaha kutoka ndani ya moyo wangu… sina chuki wala ghadhabu yoyote kutokana na hayo yaliyosemwa.
“Kinyume chake, naomba tumwombee au tuwaombe wote waliohusika na maneno kama hayo kusudi mwenyezi Mungu aweze kutuliza na kudumisha amani katika taifa letu.
“Kama viongozi wa wa Serikali au wale wenye mamlaka wanafanya kitu, ni juu yao na wajibu wao, narudia kusema sina chuki na neno langu ni msamaha kwa wale wote waliokuwa na maneno yasiokuwa na tija, tumsifu Yesu Kristo,”alisema Kardinali Pengo.

Asimulia makosa
Kuhusu kesi iliyofunguliwa, Mchungaji Mwangasa alisema walipofika polisi walikuta Askofu Gwajima ameshtakiwa kwa makosa mawili huku moja likiwa la jinai likihusu kutoa matusi hadharani na kosa la pili likiwa ni kumtukana Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Muadhama Polycap Kardinali Pengo.

Kuhusu afya ya Askofu Gwajima, inasemekana kuwa hali yake imeendelea kuimarika tofauti na alipofikishwa hospitalini hapo siku nne zilizopita.
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jana, mke wa Askofu Gwajima,Grace Gwajima alisema afya ya mume wake imeanza kuimarika, licha ya kuendelea kulazwa chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).
Alisema kama hali ikiendelea hivyo mpaka leo, watafanya utaratibu wa kumtoa ICU na kumhamishia chumba cha kawaida.
“Askofu anaendelea vizuri,anaongea na anaweza kula leo (jana)… tunamshukuru Mungu kwa hilo,” alisema Grace.
Askofu Gwajima,alizimia mwishoni mwa wiki wakati akihojiwa katika kituo Kikuu cha Polisi mjini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutoa lugha za matusi na kashfa dhidi ya Kardinali Pengo.
Katika hatua nyingine, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo amevunja ukimya na kusema amemsamehe kutoka moyoni Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Kardinali Pengo ametoa kauli hiyo, ikiwa ni siku chache tu baada ya Askofu Gwajima kumshambulia kwa maneno makali yaliyosababisha aitwe polisi kuhojiwa.
Kardinali Pengo, alitoa kauli hiyo,wakati wa mahubiri ya misa takatifu ya matawi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu mjini Dar es Salaam jana.
“Sina kinyongo na Askofu Gwajima na kwamba nimemsameha kwa yote aliyosema.
“Ndugu zangu waamini naomba kueleza au kutamka kwa kila mmoja wenu kuhusu maneno yaliyozuka hivi karibuni.
“Kutoka ndani ya moyo wangu kwa yeyote aliyesema hayo,mimi natoa msamaha kutoka ndani ya moyo wangu… sina chuki wala ghadhabu yoyote kutokana na hayo yaliyosemwa.
“Kinyume chake, naomba tumwombee au tuwaombe wote waliohusika na maneno kama hayo kusudi mwenyezi Mungu aweze kutuliza na kudumisha amani katika taifa letu.
“Kama viongozi wa wa Serikali au wale wenye mamlaka wanafanya kitu, ni juu yao na wajibu wao, narudia kusema sina chuki na neno langu ni msamaha kwa wale wote waliokuwa na maneno yasiokuwa na tija, tumsifu Yesu Kristo,”alisema Kardinali Pengo.
Source:Mtanzania