Hatimaye safari ya mwisho ya George ‘Bonge’ Njabili wa Mtoni "Lulu” Choir imekamilika baada ya mwili wake kurudishwa udongoni kwenye makaburi ya Kibumbe, Kiwira Mkoani Mbeya majira ya saa saba mchana - mara baada ya ibada ya maazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Moravian Kiwira.
Maelfu ya watu wa jiji la Mbeya wamejitokeza kwa wingi kuaga mwili wa George Njabili, idadi ambayo haikutarajiwa, na hapo ndipo ikafahamika kwamba George ni mtu wa watu, na alikuwa akikubalika.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, takribani zaidi ya watu elfu 4 walikuwepo huku wachungaji kadhaa pia wakiuaga mwili, ikiwemo Mchungaji Abiudi Misholi na Mchungaji Andulile kutoka Dar es Salaam.
Marehemu George ameacha watoto wawili na mke mmoja, Bi Tumpe. GK imefanikiwa kupata picha chache za kilichojiri kutoka kwa rafiki wa karibu wa marehemu, Mwinjilisti Danstan Mtoi, na nasi tunakufikishia.
Taarifa zilizotolewa na rais wa shirikisho la waimbaji bwana Addo November Mwasongwe kupitia ukurasa wake wa Facebook na kubainisha kwamba marehemu George alianguka akiwa nyumbani kwake maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam wakati akijiandaa kuelekea kazini tukio ambalo halikuchukua mda mrefu na mwimbaji huyo kutwaliwa kabla hajafikishwa hospitalini.
Marehemu George atakumbukwa kwa huduma yake njema ya uimbaji kupitia kwaya ya Lulu ambako aliongoza nyimbo mbalimbali ukiwemo Around the corner Jesus coming, Tazameni Upendo huu, Haleluya na nyingine nyingi huku akiipamba vyema DVD ya kwanza ya kwaya hiyo iliyobebwa na wimbo wa Lulu.

Marehemu George Njabili almaarufu kama George Bonge akiwa na mkewe enzi za uhai wake. |
Wiki iliyopita taarifa za kuhuzunisha ziliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kueleza kwamba Tasnia ya muziki wa injili imempoteza mwimbaji wake nyota na mwalimu wa kwaya ya Uinjilisti Mtoni almaarufu kama Lulu choir kutoka kanisa la Kilutheri, George Bonge Njabili aliyefariki dunia katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Taarifa zilizotolewa na rais wa shirikisho la waimbaji bwana Addo November Mwasongwe kupitia ukurasa wake wa Facebook na kubainisha kwamba marehemu George alianguka akiwa nyumbani kwake maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam wakati akijiandaa kuelekea kazini tukio ambalo halikuchukua mda mrefu na mwimbaji huyo kutwaliwa kabla hajafikishwa hospitalini.
Marehemu George atakumbukwa kwa huduma yake njema ya uimbaji kupitia kwaya ya Lulu ambako aliongoza nyimbo mbalimbali ukiwemo Around the corner Jesus coming, Tazameni Upendo huu, Haleluya na nyingine nyingi huku akiipamba vyema DVD ya kwanza ya kwaya hiyo iliyobebwa na wimbo wa Lulu.
Ni takribani miaka mitatu sasa toka aliyekuwa mwalimu mkuu wa kwaya ya Lulu kufariki dunia, kifo ambacho wengi walidhani aliyefariki ni George kiasi kwamba taarifa za kifo chake hii leo kimepokelewa kwa tofauti hasa baadhi ya watu wakidhani alishafariki siku nyingi.
source:Gospelkitaa