Majonzi yameigubika familia ya kundi maarufu la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini, baada ya mwimbaji wao wa sauti ya kwanza mahiri wa muda mrefu aitwaye Lihle Mbanjwa kufariki dunia katika ajali mbaya ya gari binafsi waliyokuwa wakisafiria huku pia mpiga ngoma (drums) maarufu wa kundi hilo Siyabulela Satsha aliyekuwemo katika gari hilo akijeruhiwa kichwani na kulazwa hospitali.
Lihle alikuwa na urafiki wa karibu sana na waimbaji waliomaliza mkataba na Joyous akiwemo Duduzile, Mahalia, Ntokozo, Hlengiwe, Brenda ilifikia mpaka wakataka kuanzisha mfuko wa pamoja wa kuwasaidia watu wenye shida. Kundi hilo limepatwa na msiba ikiwa jumamosi walifanya onyesho huko Kimberley, wiki hii wakitarajiwa kuelekea nchini Swaziland kabla ya kuelekea nchini Kenya tarehe 14 kwa onyesho lingine.
source:Gospelkitaa
Lihle akiwa na Ntokozo, Hlengiwe pamoja na Kuki ambao kwa pamoja wanaimba bendi ya Ntokozo na Nqubeko kama waitikiaji. |
source:Gospelkitaa